Friday, November 24, 2017

ZAIDI YA NG'OMBE 68,000 KUPIGWA CHAPA WILAYA YA HAI

Katibu Tawala Wilaya ya Hai Upendo Wella akipiga chapa moja ya ng'ombe kama ishara ya kuzindua zoezi la kupiga chapa mifugo. (Picha na Davis Minja)


NA Omary Mlekwa
HAI.


ZAIDI ya Ng’ombe elfu 68 zinatarajiwa kupigwa chapa katika zoezi lililoanza kwenye Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro  ili kutekeleza Agizo la wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo linatarajiwa kukamilika Desemba 30 mwaka huu.

Friday, November 10, 2017

WATUMISHI WATORO KUWAJIBISHWA KINIDHAMU

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Ndugu Yohana Elia Sintoo akizungumza na watumishi wa Halmashauri yake walioripoti vituo vya kazi wakitoka masomoni. (Picha na Riziki Lesuya)

Na. Adrian Lyapembile
HAI

Tabia ya kuchelewa kuripoti vituo vya kazi kwa watumishi wa umma wanaopewa ruhusa kwenda masomoni imekemewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo.

Monday, November 6, 2017

MKURUGENZI HAI AHIMIZA WATUMISHI KUTUMIA SACCOSS KUJIENDELEZA KIUCHUMI


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Ndugu Yohana Elia Sintoo (Picha kutoka Maktaba)


Na. Adrian Lyapembile
HAI


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai  Yohana Elia Sintoo amewataka wafanyakazi wa Umma katika Wilaya za Hai na Siha kushirikiana kwa kutumia vyama vya ushirika kwani ndiyo suluhisho halisi la maswala ya kiuchumi.

NAIBU KATIBU MKUU APONGEZA USTAWI WA JAMII WILAYA YA HAI


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ndugu Hassan Khatib Hassan (Waliokaa aliyevaa Suti) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa timu ya Ulinzi wa Mtoto Wilaya ya Hai alipotembelea Dawati la Jinsia na Watoto Kituo cha Polisi Wilaya ya Hai. (Picha na Edwin Lamtey)



Na Adrian Lyapembile
HAI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ndugu Hassan Khatib Hassan ametoa pongezi kwa kitengo cha Ustawi wa Jamii Wilaya ya Hai kwa utendaji mzuri na utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo swala la ulinzi wa mtoto.

Wednesday, October 11, 2017

WAFUGAJI WANOLEWA KUONGEZA UPATIKANAJI MAZIWA


Na. Riziki Lesuya  
HAI

Meneja mradi wa maziwa kutoka Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) Thom Olesika akizungumza na washiriki wa mafunzo kwa wafugaji (hawapo pichani)

Wafugaji  katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuthamini na kutunza miradi ya maendeleo inayoanzishwa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili miradi hiyo iweze kudumu na kuleta tija kwa jamii kama ilivyokusudiwa.

MATUMIZI YA MFUMO WA KIELEKTRONIKI KUONDOA CHANGAMOTO HUDUMA ZA AFYA

Na. Latifa Botto  
HAI

Matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa kutolea huduma za afya (GOT HOMIS)  ulioboreshwa utasaidia juhudi za kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo mahospitalini ikiwa ni pamoja na kudhibiti upotevu wa mapato.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Yohana Sintoo  (aliyevaa suti) akiwa na washiriki wa mafunzo ya mfumo ya kielektroniki wa huduma za afya.

Wednesday, August 2, 2017

MKURUGENZI WA WILAYA YA HAI AWATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI

Baadhi ya wanawake waliohudhuria Uzinduzi wa Baraza la Kuwezasha Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Hai, wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi. 


HAI - KILIMANJARO

WANAWAKE wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa za kiuchumi zinapojitokeza kwani maendeleo yaangalii jinsia ya mtu bali namna mtu anavyojituma na kujishughulisha.


Tuesday, June 6, 2017

TUNZENI MAZINGIRA - KATIBU TAWALA

Na Stella MMbando
HAI

Wananchi wa Wilaya ya Hai wamehimizwa kuhifadhi na kutunza mazingira kwa kuotesha miti  ili kuepukana na athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira kama ukame.

"ASANTE BABA KWA VITANDA NA MAGODORO" : WANANCHI WA HAI

Baadhi ya vitanda na magodoro yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano  Dkt. John Pombe Magufuli kwa Wilaya ya Hai (Picha zote na Davis Minja)


Na Davis Minja
HAI

Hospitali ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro imepokea msaada wa vitanda 25 magodoro na shuka yake toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la utoaji na uboreshaji wa huduma za afya.

Friday, June 2, 2017

WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI KWA FEDHA ZA TASAF

Bi Asha afisa wa kata ya Masama Kusini akitoa mafunzo kwa wanufaika wa TASAF kabla ya kuanza zoezi la kuhawilisha fedha


Na Stella Mmbando
HAI

Wananchi wa Kijiji cha Lemira Kati kata ya Masama Kati wilayani Hai wameishukuru serikali kwa fedha inazotoa kusaidia kaya masikini nchini na kuomba kuongezwa idadi ya wanufaika kwa kuwa bado zipo familia nyingi hazijaweza kukidhi mahitaji.

WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

Diwani wa Kata ya Masama Mashariki  John Munis akikabidhi zawadi 
kwa wanafunzi waliofanya vizuri


Na Elizabeth Mafie

HAI

Wito umetolewa kwa wanafunzi kote nchini kusoma kwa bidii pamoja na kumcha Mungu ili waweze kufanikiwa katika masomo yao na kufanikisha ndoto zao za kielimu.


Thursday, January 26, 2017

SERIKALI YAITAKA JAMII KUSHIRIKI MAENDELEO



 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick akipokea mchango wa bati kutoka kwa Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Salie Mlay. (Picha zote na Adrian Lyapembile)

RC KILIMANJARO ASHAURI FEDHA ZA MIRADI ZIZINGATIE MAZINGIRA

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick akipokea taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu kwenye shule ya sekondari Kikafuu kutoka kwa Mkuu wa Shule hiyo. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo.                                      (Picha zote na Adrian Lyapembile)

Friday, January 20, 2017

Tuesday, October 4, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA: MWENGE WA UHURU 2016 WILAYANI HAI-KILIMANJARO

Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Siha Onesmo Buswelu

DC AHIMIZA UBUNIFU KWA WATUMISHI WA UMMA



Na: Stella Mmbando -  HAI

Mkuu wa Wilaya ya Hai  Gelasius Byakanwa amewataka wakuu wa idara na watumishi wote wa Wilaya hiyo  kujituma na kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao idara zao ili kuongeza ufanisi na kuimarisha ari ya kufanya kazi kwa maendeleo ya taifa.

Byakanwa alizungumza hayo wakati wa kutoa tuzo za mshindi wa shindano la ubunifu kwa idara na vitengo vya halmashauri hiyo ambapo mwezi huu zimeshindanishwa idara tatu ikiwamo idara ya mapato, biashara na mazingira.


Thursday, June 4, 2015

MKURUGENZI AUSHUKURU UONGOZI WA CHAMA CHA MSALABA MWEKUNDU




MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Said Ahmed Said Mderu ameushukuru uongozi wa chama cha msalaba mwekundu kwa msaada walioutoa kwa wananchi walioathirika na mafuriko katika baadhi ya vijiji vya Kata za Weru weru,Masama Rundugai na Mnadani.

Akipokea misaada hiyo Mderu amewataka wananchi waliopata msaada huo kuitunza na kuitumia ili kuwasaidia katika kipindi hiki kigumu.


Mderu amesema kuwa  ikiwa wahanga hao wa mafuriko watakuwa wanatumia misaada wanayo pelekewa pasipo utaratibu maalumu utasababisha mashirika mengine pamoja na wadau mbalimbali kusitisha kupeleka hudumu muhimu maeneo hayo ,hivyo ni vema waka onesha hali ya ustaarabu katika kutumia misaada

Kwa upande mwingine wamewaomba wadau mbali mbali kuendelea kujitokeza kuwasaidia wananchi hao ambao hadi waliathirika na mafuriko yaliyosababisha kaya 50 kukosa sehemu za kukaa.

Chama cha Msalaba Mwekundu Mkoani Kilimanjaro kilitoa misaada mbali mbali kwa wananchi hao ikiwa ni pamoja na Mablanketi,Ndoo,beseni,Vyandarua na dawa ya kutibia maji ya water guard.

Awali akikabidhi misaada hiyo mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Kilimanjro August Temu

NMB YATOA MSAADA

MKUU WA WILAYA AMPONGEZA ASKOFU



MKUU wa wilaya ya Hai Antony Mtaka amempongeza aliyekuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Askofu Mstaafu Erasto N kweka  kwa jitihada zake alizozifanya wakati akihudumu kama askofu ikiwamo kupokea miradi mbli mbali ya maji iliyopitia katika Dayosisi Hiyo.

Mtaka ameyasema hivi karibuni wakati wa kikao cha  kumchagua mwenyekiti na wajumbe wa bodi ya maji ya Lyamungo Umbwe kilichofanyika katika shule ya sekondari Lyamungo.

Amesema kuwa ni mfano wa kuigwa kwa kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele katika kuiletea jamii maendeleo pasipokuwa na ukiritimba, ubadhirifu na kuweka maslai binafsi ya shughuli za kimaendeleo.

“ ni jambo la bahati sana kwa Askofu Kweka kutanguliza maslai ya Wananchi katika mradi huu wa maji pasipo kujali atanufaika vipi, ingekuwa ni mtu asiyekuwa mwadilifu angegeuza mradi kuwa wake huku wananchi wakiangamia kwa ukosefu wa maji safi na salama.” Alisema Mtaka

“Askofu Kweka alipoke Euro mill. 34 sawa na shilingi Bill. 68 mwaka 1992 ambapo ndipo mradi huo ulianza rasmi ukijumuisha vijiji 11 kutoka Hai na Vijiji 13 kutoka Moshi vijijini, ingekuwa ni mwingine angepeleka wapi?”  Alihoji Mtaka

Sanjari na hayo amewataka viongozi wapya waliochaguliwa kuiongoza bodi hiyo ya Lyamungo Umbwe kuepuka kuchanganya siasa na kazi za miradi ya maendeleo ili miradi hiyo iweze kuwanufaisha wananchi wote na vizazi vya baadae.

“epukeni kutapeliwa na wanasiasa wanaojiingiza katika miradi ya kimaendeleo kwani wengi wao ni wapotoshaji kwa kuingiza siasa katika utendaji” alisema Mtaka.


Kwa upande wake mhandisi wa maji wilaya ya Hai ambaye pia alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo Mhandisi Nyakaraita Mwita amewataka wajumbe waliochaguliwa katika bodi hiyo kupeanan ushirikianano katika utendaji ikiwemo pamoja na kushirikiana na halmashauri ili kuleta ufanisi zaidi.

Ameongeza kuwa jamii inatakiwa kuopata maji safi na salama kama bodi ya maji ilivyojusudia ili kuepuka mnagonjwa mbali mbali yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo safi na salama.

Pia amesema kuwa wanawake wamekuwa ni waathirika wakubwa wa utafutaji wa maji safi na salama katika familia zao jambo linalowapelekea kushindwa kushiriki katika  shughuli nyingine za kimaendeleo.

Katika zoezi la upigaji wa kura wajumbe walikuwa 258 ambapo kura moja iliharibika huku Michael Sitaki Mmasy akishikilia nafasi ya mwenyekiti,Emmanuel Izack Show akiwa ni makamu mwenyekiti ambapo walipita bila kupingwa kutokana na kutojitokeza kwa wagombea wengine kuchukua fomu za nafasi hizo kama ilivyotakiwa.


Kwa upande wa wajumbe watendaji wa bodi ya maji, Bibianna Mmasy aliibuka mshindi kwa kupata kura 85 na Bi, Joyce Kweka akipata kura 71 ambazo zote kwa pamoja zilivuka asilimia hamsini iliyoitajika.
kaika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Ndg Antony Mtaka akizungumza katika uchaguzi wa wajumbe wa bodi ya maji ya Lyamungo Umbwe


 MKUU WA WILAYA YA HAI NDUGU ANTONY MTAKA AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE





 MHANDISI WA MAJI WILAYA MWITA NYAKARAITA AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE