MKUU wa wilaya ya Hai Antony Mtaka
amempongeza aliyekuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Askofu Mstaafu
Erasto N kweka kwa jitihada zake alizozifanya wakati akihudumu
kama askofu ikiwamo kupokea miradi mbli mbali ya maji iliyopitia katika
Dayosisi Hiyo.
Mtaka ameyasema hivi karibuni wakati
wa kikao cha kumchagua mwenyekiti na wajumbe wa bodi ya maji ya
Lyamungo Umbwe kilichofanyika katika shule ya sekondari Lyamungo.
Amesema kuwa ni mfano wa kuigwa
kwa kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele katika kuiletea jamii maendeleo
pasipokuwa na ukiritimba, ubadhirifu na kuweka maslai binafsi ya shughuli za
kimaendeleo.
“ ni jambo la bahati sana kwa
Askofu Kweka kutanguliza maslai ya Wananchi katika mradi huu wa maji pasipo
kujali atanufaika vipi, ingekuwa ni mtu asiyekuwa mwadilifu angegeuza mradi
kuwa wake huku wananchi wakiangamia kwa ukosefu wa maji safi na salama.”
Alisema Mtaka
“Askofu Kweka alipoke Euro mill.
34 sawa na shilingi Bill. 68 mwaka 1992 ambapo ndipo mradi huo ulianza rasmi
ukijumuisha vijiji 11 kutoka Hai na Vijiji 13 kutoka Moshi vijijini, ingekuwa
ni mwingine angepeleka wapi?” Alihoji Mtaka
Sanjari na hayo amewataka viongozi
wapya waliochaguliwa kuiongoza bodi hiyo ya Lyamungo Umbwe kuepuka
kuchanganya siasa na kazi za miradi ya maendeleo ili miradi hiyo iweze
kuwanufaisha wananchi wote na vizazi vya baadae.
“epukeni kutapeliwa na wanasiasa
wanaojiingiza katika miradi ya kimaendeleo kwani wengi wao ni wapotoshaji kwa
kuingiza siasa katika utendaji” alisema Mtaka.
Kwa upande wake mhandisi wa maji
wilaya ya Hai ambaye pia alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo Mhandisi
Nyakaraita Mwita amewataka wajumbe waliochaguliwa katika bodi hiyo kupeanan
ushirikianano katika utendaji ikiwemo pamoja na kushirikiana na halmashauri
ili kuleta ufanisi zaidi.
Ameongeza kuwa jamii inatakiwa
kuopata maji safi na salama kama bodi ya maji ilivyojusudia ili kuepuka
mnagonjwa mbali mbali yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo safi na salama.
Pia amesema kuwa wanawake wamekuwa
ni waathirika wakubwa wa utafutaji wa maji safi na salama katika familia zao
jambo linalowapelekea kushindwa kushiriki katika shughuli nyingine
za kimaendeleo.
Katika zoezi la upigaji wa kura
wajumbe walikuwa 258 ambapo kura moja iliharibika huku Michael Sitaki Mmasy
akishikilia nafasi ya mwenyekiti,Emmanuel Izack Show akiwa ni makamu
mwenyekiti ambapo walipita bila kupingwa kutokana na kutojitokeza kwa
wagombea wengine kuchukua fomu za nafasi hizo kama ilivyotakiwa.
Kwa upande wa wajumbe watendaji wa
bodi ya maji, Bibianna Mmasy aliibuka mshindi kwa kupata kura 85 na Bi, Joyce
Kweka akipata kura 71 ambazo zote kwa pamoja zilivuka asilimia hamsini
iliyoitajika.
|
Thursday, June 4, 2015
MKUU WA WILAYA AMPONGEZA ASKOFU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment