Katibu Tawala Wilaya ya Hai Upendo Wella akipiga chapa moja ya ng'ombe kama ishara ya kuzindua zoezi la kupiga chapa mifugo. (Picha na Davis Minja) |
NA Omary Mlekwa
HAI.
ZAIDI ya
Ng’ombe elfu 68 zinatarajiwa kupigwa chapa katika zoezi lililoanza kwenye
Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro
ili kutekeleza Agizo la wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo linatarajiwa
kukamilika Desemba 30 mwaka huu.
Hayo yamebaishwa
na Katibu Tawala Wilaya ya Hai Upendo Wella wakati akizungumza na wafugaji wa kijiji cha Sanya
Station Kata ya Kia alipotembelea zoezi hilo pamoja na kufanya uzinduzi huo.
Alisema
kuwa kuna kila sababu kwa wakazi wa wilaya ya Hai haswa wafugaji kujitokeza kwa
wingi kushiriki zoezi hilo ili kuwezesha wanyama wao kupigwa chapa kutokana na
umuhimu wa zoezi hilo.
“kukamilika
kwa zoezi hili itasaidia kutambua mifugo iliyopo kwani wilaya imekuwa na
migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji kutokana na wimbi kubwa
la mifugo kutoka wilaya za jirani na hata wafugaji kutoka nje kuvamia mashamba ya wakulima kwa ajili ya
malisho.”Alisema Wella.
Hata
hivyo aliwataka wafugaji wote kutoa mifugo yao na kupigwa kwa muda huu na mara
baada ya kukamilika kwa zoezi hilo wataanza kuwachukulia hatua wale ambao
watashindwa kutekeleza agizo hilo.
Kupande
wake afisa mifugo wa wilaya ya Hai, Elia Machange amesema kuwa tangu kuanza kwa
zoezi hilo wamekutana na muitikio mkubwa kutoka kwa wafugaji ambao wamepeleka
mifugo yao kupigwa chapa.
Aidhani
amesema kutokana na matumizi makubwa ya kuni wamejipanga kuhakikisha kuwa zoezi
hilo halikwami kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji kutoa ushirikiano wao wa
ili kukabiliana tatizo hilo na huduma
iendeele kutolewa kwa muda wote.
Kwa
upande wake Mfugaji Yohana Laizer alisema zoezi hilo litasaidia kuwatambua ngombe watakaovamia maeneo yao kwani mifugo
yao itakuwa na chapa ya wilaya ya Hai,huku wizi wa mifugo ukidhibitiwa kwa
kiasi kikubwa wakati wa mifugo yao ikihama kutafuta malisho.
Ameongeza
kuwa kupigwa chapa kwa Ng’ombe hao
itasaidia kuondoa mwingiliano wa mifugo kwa wilaya nyingine jambo ambalo
litawasaidia katika kuhifadhi sehemu za malisho.
No comments:
Post a Comment