Friday, June 2, 2017

WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

Diwani wa Kata ya Masama Mashariki  John Munis akikabidhi zawadi 
kwa wanafunzi waliofanya vizuri


Na Elizabeth Mafie

HAI

Wito umetolewa kwa wanafunzi kote nchini kusoma kwa bidii pamoja na kumcha Mungu ili waweze kufanikiwa katika masomo yao na kufanikisha ndoto zao za kielimu.


Wito huo ulitolewa  na Diwani wa Kata ya Masama Mashariki mheshimiwa John Munis wakati alipotembelea shule mbili za sekondari  zilizopo katika kata yake ambazo ni Marire  na Sawe na kuwapongeza walimu kwa kufundisha kwa bidii pamoja na wanafunzi waliofaulu vizuri katika masomo mbalimbali.

Akikabidhi zawadi kwa wanafunzi hao Mh. Munisi alisema kuwa anatambua jitihada zinazofanywa na walimu hao katika kufanikisha ufaulu, na kuwataka wanafunzi wote kuongeza bidii katika masomo na kuwaahidi kuwa wanafunzi wote watakaofaulu kwa daraja la kwanza watapata zawadi bila kujali wingi wao.

Alisema kuwa kila mmoja akitambua wajibu wake akiwemo mzazi, mwalimu na mwanafunzi  ufaulu utaongezeka kwa asilimia kubwa na kusisitiza kila mmoja kutenda kwa haki .

Kwa upande wake diwani wa kata ya Machame Uroki Robsoni Kimaro  aliwapongeza walimu wa shule hizo kwa kufundisha kwa bidii bila kujali changamoto wanazokutana nazo  huku akiwataka wanafuzi  kuongeza bidii ya kusoma pamoja na kuepuka  matendo maovu ikiwepo ngono na unywaji wa pombe.

Nae mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Marire Dkt Abisai Masawe  na Mkuu wa shule hiyo mwalimu Namkanda Kagonji wamewashukuru madiwani hao kufika katika shule zao huku wakiahidi kutekeleza mikakati yote waliyoipanga.


Diwani wa Kata ya Masama Mashariki  John Munis akikabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri

No comments:

Post a Comment