Friday, June 2, 2017

WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI KWA FEDHA ZA TASAF

Bi Asha afisa wa kata ya Masama Kusini akitoa mafunzo kwa wanufaika wa TASAF kabla ya kuanza zoezi la kuhawilisha fedha


Na Stella Mmbando
HAI

Wananchi wa Kijiji cha Lemira Kati kata ya Masama Kati wilayani Hai wameishukuru serikali kwa fedha inazotoa kusaidia kaya masikini nchini na kuomba kuongezwa idadi ya wanufaika kwa kuwa bado zipo familia nyingi hazijaweza kukidhi mahitaji.

Ombi hilo limetolewa na  baadhi ya wananchi  waliopo katika mradi wa kuwezesha kaya maskini unaowezeshwa na TASAF wakati wa zoezi la kugawa fedha katika Kijiji cha Lemira Kati.

Akiongea kwa niaba ya wenzake bi Aikande Tonga alisema fedha walizopewa na TASAF zimewawezesha kuanzisha miradi mbalimbali ya kuwaingizia kipato huku akitolea mfano wake yeye  ambaye ameweza kuanzisha mradi wa kufuga kuku ambao umemsaidia kuweza kulipia ada ya shule ya watoto.


Aidha Mwenyekiti wa kijiji cha Lemira kati ndugu Akao Swai  ambaye pia ni mratibu wa  mpango wa kusaidia kaya maskini kijijini humo alisema  watu  wengi wamenufaika na mradi huo  ambao umewawezesha kuanzisha miradi ya kilimo na ufugaji ambapo baadhi yao wanachangiana na kufanya shughuli za kichumi.

Aliyesimama mbele , bi Asha afisa wa kata ya Masama Kusini akitoa mafunzo kabla ya zoezi la kugawa fedha

aliyenyoosha Mkono  Mwenyekiti wa kijiji cha Masama Lemira ndugu  Akao Swai alipokuwa akiuliza swali

No comments:

Post a Comment