Tuesday, June 6, 2017

TUNZENI MAZINGIRA - KATIBU TAWALA

Na Stella MMbando
HAI

Wananchi wa Wilaya ya Hai wamehimizwa kuhifadhi na kutunza mazingira kwa kuotesha miti  ili kuepukana na athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira kama ukame.

Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Hai  Upendo Wella wakati wa zoezi la kupanda miti katika kijiji cha Chemka ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki  ya mazingira duniani ambapo kwa Wilaya maadhimisho hayo yalihitimishwa kwa zoezi hilo la kupanda miti.

Bi Wella aliwapongeza viongozi wa kijiji kwa kulinda mazingira na kuwaomba wananchi kuendelea  kutunza mazingira hayo kupitia kivutio hicho kinachoingiza kipato kwa serikali .

Aliwasisitiza wananchi wa kijiji hicho kuona umuhimu wa kutunza mazingira  ili kuendelea kuongeza vyanzo vya mapato, kwakuwa chemchemi hiyo huingizia serikali ya kijiji hicho fedha kupitia kwa watalii wanaotembelea eneo hilo.

Alisema upandaji miti pia husaidia kulinda vyanzo vya maji na kuwaagiza wananchi kuhakikisha kuwa kila mmoja anapanda miti zaidi ya nane.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Hai Yohana Elia Sintoo (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chemka kwenye maadhimisho ya Siku ya Mazingira


 Katibu Tawala Wilaya bi Upendo Wella akipanda mti katika maadhimisho ya wiki ya mazingira



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai ndugu Yohana Elia Sintoo akipanda mti katika maadhimisho ya siku ya mazingira (Picha zote na Adrian Lyapembile)


No comments:

Post a Comment