Eneo linalotumiwa na Mh. Freeman Mbowe kwa shughuli za kilimo (Kilimanjaro Veggies) |
Eneo linalotumiwa na Mh. Freeman Mbowe kwa shughuli za kilimo (Kilimanjaro Veggies) |
Sehemu ya eneo la shughuli za kilimo katika shamba la Kilimanjaro Veggie |
Mkuu wa Wilaya ya Hai Gellasius Byakanwa akitoa maelekezo ya serikali kwa mmiliki wa shamba |
Na Davis J. Minja
HAI - KILIMANJARO
MKUU wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Gellasius Byakanwa,
amesitisha shughuli za kilimo katika shamba la Kilimanjaro Veggies linalomikiwa
na Mbunge wa jimbo la Hai Freeman Mbowe kutokana na shamba hilo kuwa ndani ya
chanzo cha maji ya mto Weruweru.
Byakanwa alitoa amri hiyo baada ya kutembelea shamba hilo
lenye ukubwa za zaidi ya ekari mbili
lililoko kijiji cha Nshara na kukuta kumeanzishwa shughuli za kilimo ndani ya
chanzo cha maji kinyume na sheria na kufanya uharibifu wa mazingira.
Alisema Mbunge huyo amefanya uharibifu wa mazingira kwa
kuvuna miti ya asili bila kibali cha Mkuu wa Wilaya kulingana na maamuzi ya
kamati ya Ushauri ya mkoa (RCC) pamoja na kuvuta maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za
utumiaji wa maji ya mfereji.
Alifafanua kuwa mnamo Januari 10 mwaka huu, alifanya ziara
katika shamba hilo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi pamoja na
Mamlaka ya bonde la maji Mto Pangani na kujionea hali halisi ambapo alimwandikia
Mbowe barua ya wito wa kufika ofisi ya mkuu wa wilaya mnamo Januari 13 akiwa na
vibali vinavyomruhusu kufanya shughuli za kibinadamu katika eneo hilo.
Akizungumza kuhusiana na shughuli za kilimo katika eneo
hilo, Nelly Mbowe ambaye ni dada wa Mbunge Freeman Mbowe anayesimamia shughuli
hizo amekiri kufikisha taarifa kwa mbunge kuhusiana na wito aliopewa na Mkuu wa
Wilaya.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa Kijjiji cha Nshara Emanueli Mbowe alisema shughuli za kilimo
katika eneo hilo zilianza mwaka jana ambapo alielezwa kuwa Mbowe anataka
kuendeleza kilimo katika sehemu hiyo na anavyo vibali vyote zinavyomruhusu
kufanya shughuli hiyo.
No comments:
Post a Comment