Tuesday, June 6, 2017

"ASANTE BABA KWA VITANDA NA MAGODORO" : WANANCHI WA HAI

Baadhi ya vitanda na magodoro yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano  Dkt. John Pombe Magufuli kwa Wilaya ya Hai (Picha zote na Davis Minja)


Na Davis Minja
HAI

Hospitali ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro imepokea msaada wa vitanda 25 magodoro na shuka yake toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la utoaji na uboreshaji wa huduma za afya.


Akikabidhi vitanda hivyo Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa amesema kuwa serikali imekuwa ikiangalia sekta muhimu kwa kuziboresha ikiwa ni pamoja na kufanya sekta hizo kutoa huduma zinazo hitajika na kuridhisha ikiwamo sekta ya Afya.

Ameongeza kuwa ili kuweza kuwa na Taifa linalo jikita katika kuimarisha sekta ya Viwanda kama agizo la Rais linavyosema ni vema wananchi wakawa na Afya njema na imara zitakazo weza kufanya kazi na kuwekeza katika viwanda.

Aidha amemshukuru Rais kwa kutambua umuhimu wa kuendelea kutoa vifaa tiba katika hosipitali,huku akiwataka wananchi kuvitunza vifaa tiba vinavyo tolewa katika hospitali,vituo vya afya na Zahanati.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Yohana Sintoo ameshukuru hatua hiyo ya  Rais kuboresha  sekta ya Afya hususani katika vifaa tiba ambavyo vimekuwa ni changamoto kwa hospitali, vituo vya afya na zahanati kwa baadhi ya maeneo.

Aidha amewataka watendaji katika hospitali hiyo pamoja na wagonjwa kutunza vifaa tiba vinavyo tolewa katika maeneo yao ili kuweza kutumika kwa muda mrefu hali itakayo weza saidia kupunguza changamoto za lazima na zisizo za lazima.

Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu wa hospitali hiyo Bernadetha Swai ametaja msaada wa vitanda walivyo pokea kuwa ni vitanda 25, vikiwa na shuka na magodoro kati ya hivyo vitanda 20 ni vya kawaida na vitanda 5 ni maalumu kwaajili ya kujifungulia akina mama wajawazito vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 16.

Kwa upande wao wananchi wa Wilaya hiyo wameshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  kwa kutoa vitanda hivyo ambavyo vitasaidia kupunguza tatizo la uhaba vya vitanda katika wodi ya wakina mama wajawazito.



Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Hai Yohana Elia Sintoo moja ya vitanda na godoro.
Baadhi ya vitanda na magodoro yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano  Dkt. John Pombe Magufuli kwa Wilaya ya Hai (Picha zote na Davis Minja)




No comments:

Post a Comment