MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Said Ahmed Said Mderu ameushukuru uongozi wa chama cha msalaba mwekundu kwa msaada walioutoa kwa wananchi walioathirika na mafuriko katika baadhi ya vijiji vya Kata za Weru weru,Masama Rundugai na Mnadani. |
Akipokea misaada hiyo Mderu
amewataka wananchi waliopata msaada huo kuitunza na kuitumia ili kuwasaidia
katika kipindi hiki kigumu.
Mderu amesema kuwa ikiwa
wahanga hao wa mafuriko watakuwa wanatumia misaada wanayo pelekewa pasipo
utaratibu maalumu utasababisha mashirika mengine pamoja na wadau mbalimbali
kusitisha kupeleka hudumu muhimu maeneo hayo ,hivyo ni vema waka onesha hali ya
ustaarabu katika kutumia misaada
Kwa upande mwingine wamewaomba wadau
mbali mbali kuendelea kujitokeza kuwasaidia wananchi hao ambao hadi
waliathirika na mafuriko yaliyosababisha kaya 50 kukosa sehemu za kukaa.
Chama cha Msalaba Mwekundu Mkoani
Kilimanjaro kilitoa misaada mbali mbali kwa wananchi hao ikiwa ni pamoja na
Mablanketi,Ndoo,beseni,Vyandarua na dawa ya kutibia maji ya water guard.
Awali akikabidhi misaada hiyo mwenyekiti
wa Chama hicho Mkoa wa Kilimanjro August Temu
No comments:
Post a Comment