Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick akiongozana akitembelea jengo la darasa kwenye shule ya Sekondari KIA wilayani Hai lilijengwa kupitia mredi wa SEDEP |
Jengo la vyumba vya madarasa kwenye shule ya sekondari KIA wilayani Hai lililojengwa kupitia mradi wa SEDEP |
Jengo la choo cha walimu kwenye shule ya sekondari Kyuu wilayani Hai |
Mhandisi Msangi wa wilaya ya Hai akitoa taarifa ya ujenzi wa vyoo kwenye shule ya sekondari Kyuu kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick |
Jengo la vyumba vya madarasa kwenye shule ya sekondari Kyuu lililojengwa kupitia mradi wa SEDEP |
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kikafuu wilayani Hai iliyofaidika na ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba ya walimu vilivyojengwa kupitia mradi wa SEDEP |
Na Davis J. Minja
HAI -
KILIMANJARO
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick ameiomba
serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na TAMISEMIi
kuangalia upya gharama za ujenzi wa majengo katika miradi hasa mradi wa SEDEP kuzingatia mazingira ya maeneo wanapopeleka
mradi ili kiasi cha fedha kinachotolewa kiweze kutosheleza miradi hiyo.
Ametoa wito huo leo wakati wa ziara yake ya kutembelea
takribani miradi minne katika shule za sekondari Wilayani Hai Mkoani humo kwa
lengo la kukagua hatua zilizofikiwa katika miradi hiyo kwa fedha zilizo tolewa
na serikali kwa ajili ya kuboresha huduma katika shule.
Sadick emezitaja shule zilizofaidika na mradi wa SEDEP kuwa
ni pamoja shule ya sekondari KIA, shule ya sekondari Kyuu pamoja na shule ya
sekondari Kikafuu ambapo kati ya shule hizo baadhi zimefanyiwa maboresho ya
vyoo vya wanafunzi na waalimu na kuongezewa vyumba vya madarasa pamoja na
nyumba za waalimu.
Hivyo ameishauri wizara kufanya maamuzi ya kuelekeza fedha
hizo kwa halmashauri kutumia force akaunti ili kuweza kujenga majengo kwa
gharama nafuu kwa kuwatumia wakandarasi wa wilaya kutokana na wakandarasi wanaopokea
tenda kuwa na gharama kubwa huku kiasi kinachotolewa na wizara kuwa kidogo.
No comments:
Post a Comment