Friday, April 6, 2018

Wananchi Watakiwa Kutunza Miti Wanayootesha


Mkuu wa Wilaya ya Hai, Onesmo Buswelu akipanda mti kuashiria uzinduzi wa wiki ya kupanda miti uliofanyika Kijiji cha Mtakuja tarehe 05 Aprili 2018.
(Picha zote na Adrian Lyapembile)

Na Hellen Shayo
HAI

MKUU wa wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Onesmo Buswelu amewataka wananchi kutunza miti inayooteshwa katika kipindi hiki cha mvua ili iweze kukua na kukabiliana na hali ya ukame kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Thursday, March 1, 2018

NAIBU WAZIRI MABULA AAGIZA WADAIWA SUGU KODI YA ARDHI WALIPE


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anjelina Mabula akisalimiana na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Hai Onesmo Buswelu alipowasili kwenye ziara ya kikazi katika Wilaya ya Hai.


Na. Davis Minja
HAI

Naibu Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Anjelina Mabula ameitaka idara ya ardhi Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, kutowafumbia macho wadaiwa sugu waliogoma au kuchelewa kulipia kodi ya ardhi wanazomiliki.

Wednesday, February 21, 2018

WALIMU WANOLEWA KUTUNZA MLIMA KILIMANJARO


Afisa maliasili Wilaya ya Hai Mbayani Mollel akitoa mafunzo juu ya mazingira kwa waalimu wa mazingira kutoka shule 25 wilayani Hai. (picha zote na praygod Munisi)

Monday, February 12, 2018

AFISA ELIMU AAGIZA KUANZISHWA JUKWAA LA WAZAZI SHULENI


Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Hai Julius Kakyama akisisitiza jambo kwenye kikao cha wazazi wa wanafunzi kwenye shule ya sekondari Hai. (Picha zote na Praygod Munisi)


Na. Praygod Munisi
HAI

Wakuu washule za sekondari za serikali katika wilaya  ya  Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuanzisha jukwaa la wazazi na walimu ndani ya mwezi mmoja ikiwa ni sehemu ya kutekeleza majukumu yao ili kutoa nafasi ya kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya shule na wanafunzi.

Wednesday, January 3, 2018

HAI YAPONGEZWA KWA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA AFYA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akikagua miradi ya maendeleo katika hospitali ya wilaya ya Hai alipofanya ziara ya kikazi. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Hai Yohana Sintoo. (Picha na Omary Mlekwa)


Na. Adrian Lyapembile
HAI


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo ameipongeza halmashauri ya wilaya ya hai kwa kuendelea kuboresha miundombinu katika hospitali ya wilaya hiyo itakayofanikisha kutekeleza azma ya serikali kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wake.

Monday, December 11, 2017

NAIBU WAZIRI APONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI WILAYA YA HAI

Jengo la Bweni la Wanafunzi kwenye Shule ya Sekondari Harambee katika Wilaya ya Hai

Na. Riziki Lesuya
HAI


Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda amefurahishwa na kuridhishwa na usimamizi wa miradi ya maendeleo Wilayani Hai na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji  Yohana Sintoo  kwa usimamizi mzuri unaoendana  na thamani ya fedha iliyotumika.

MAREKEBISHO YA SHERIA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI

Naibu Waziri George Kakunda akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Harambee alipofanya ziara ya siku moja katika Wilaya ya Hai.


Na. Adrian Lyapembile
HAI

Serikali imejipanga kufanya marekebisho ya sheria ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998 ili kukabiliana na ongezeko la matukio ya  mimba kwa watoto walio chini ya miaka 18 hasa wanafunzi.

Friday, November 24, 2017

ZAIDI YA NG'OMBE 68,000 KUPIGWA CHAPA WILAYA YA HAI

Katibu Tawala Wilaya ya Hai Upendo Wella akipiga chapa moja ya ng'ombe kama ishara ya kuzindua zoezi la kupiga chapa mifugo. (Picha na Davis Minja)


NA Omary Mlekwa
HAI.


ZAIDI ya Ng’ombe elfu 68 zinatarajiwa kupigwa chapa katika zoezi lililoanza kwenye Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro  ili kutekeleza Agizo la wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo linatarajiwa kukamilika Desemba 30 mwaka huu.

Friday, November 10, 2017

WATUMISHI WATORO KUWAJIBISHWA KINIDHAMU

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Ndugu Yohana Elia Sintoo akizungumza na watumishi wa Halmashauri yake walioripoti vituo vya kazi wakitoka masomoni. (Picha na Riziki Lesuya)

Na. Adrian Lyapembile
HAI

Tabia ya kuchelewa kuripoti vituo vya kazi kwa watumishi wa umma wanaopewa ruhusa kwenda masomoni imekemewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo.

Monday, November 6, 2017

MKURUGENZI HAI AHIMIZA WATUMISHI KUTUMIA SACCOSS KUJIENDELEZA KIUCHUMI


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Ndugu Yohana Elia Sintoo (Picha kutoka Maktaba)


Na. Adrian Lyapembile
HAI


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai  Yohana Elia Sintoo amewataka wafanyakazi wa Umma katika Wilaya za Hai na Siha kushirikiana kwa kutumia vyama vya ushirika kwani ndiyo suluhisho halisi la maswala ya kiuchumi.

NAIBU KATIBU MKUU APONGEZA USTAWI WA JAMII WILAYA YA HAI


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ndugu Hassan Khatib Hassan (Waliokaa aliyevaa Suti) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa timu ya Ulinzi wa Mtoto Wilaya ya Hai alipotembelea Dawati la Jinsia na Watoto Kituo cha Polisi Wilaya ya Hai. (Picha na Edwin Lamtey)Na Adrian Lyapembile
HAI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ndugu Hassan Khatib Hassan ametoa pongezi kwa kitengo cha Ustawi wa Jamii Wilaya ya Hai kwa utendaji mzuri na utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo swala la ulinzi wa mtoto.

Wednesday, October 11, 2017

WAFUGAJI WANOLEWA KUONGEZA UPATIKANAJI MAZIWA


Na. Riziki Lesuya  
HAI

Meneja mradi wa maziwa kutoka Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) Thom Olesika akizungumza na washiriki wa mafunzo kwa wafugaji (hawapo pichani)

Wafugaji  katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuthamini na kutunza miradi ya maendeleo inayoanzishwa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili miradi hiyo iweze kudumu na kuleta tija kwa jamii kama ilivyokusudiwa.

MATUMIZI YA MFUMO WA KIELEKTRONIKI KUONDOA CHANGAMOTO HUDUMA ZA AFYA

Na. Latifa Botto  
HAI

Matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa kutolea huduma za afya (GOT HOMIS)  ulioboreshwa utasaidia juhudi za kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo mahospitalini ikiwa ni pamoja na kudhibiti upotevu wa mapato.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Yohana Sintoo  (aliyevaa suti) akiwa na washiriki wa mafunzo ya mfumo ya kielektroniki wa huduma za afya.

Wednesday, August 2, 2017

MKURUGENZI WA WILAYA YA HAI AWATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI

Baadhi ya wanawake waliohudhuria Uzinduzi wa Baraza la Kuwezasha Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Hai, wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi. 


HAI - KILIMANJARO

WANAWAKE wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa za kiuchumi zinapojitokeza kwani maendeleo yaangalii jinsia ya mtu bali namna mtu anavyojituma na kujishughulisha.


Tuesday, June 6, 2017

TUNZENI MAZINGIRA - KATIBU TAWALA

Na Stella MMbando
HAI

Wananchi wa Wilaya ya Hai wamehimizwa kuhifadhi na kutunza mazingira kwa kuotesha miti  ili kuepukana na athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira kama ukame.

"ASANTE BABA KWA VITANDA NA MAGODORO" : WANANCHI WA HAI

Baadhi ya vitanda na magodoro yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano  Dkt. John Pombe Magufuli kwa Wilaya ya Hai (Picha zote na Davis Minja)


Na Davis Minja
HAI

Hospitali ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro imepokea msaada wa vitanda 25 magodoro na shuka yake toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la utoaji na uboreshaji wa huduma za afya.

Friday, June 2, 2017

WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI KWA FEDHA ZA TASAF

Bi Asha afisa wa kata ya Masama Kusini akitoa mafunzo kwa wanufaika wa TASAF kabla ya kuanza zoezi la kuhawilisha fedha


Na Stella Mmbando
HAI

Wananchi wa Kijiji cha Lemira Kati kata ya Masama Kati wilayani Hai wameishukuru serikali kwa fedha inazotoa kusaidia kaya masikini nchini na kuomba kuongezwa idadi ya wanufaika kwa kuwa bado zipo familia nyingi hazijaweza kukidhi mahitaji.

WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

Diwani wa Kata ya Masama Mashariki  John Munis akikabidhi zawadi 
kwa wanafunzi waliofanya vizuri


Na Elizabeth Mafie

HAI

Wito umetolewa kwa wanafunzi kote nchini kusoma kwa bidii pamoja na kumcha Mungu ili waweze kufanikiwa katika masomo yao na kufanikisha ndoto zao za kielimu.