Afisa maliasili Wilaya ya Hai Mbayani Mollel akitoa mafunzo juu ya mazingira kwa waalimu wa mazingira kutoka shule 25 wilayani Hai. (picha zote na praygod Munisi) |
Mtaalamu wa kilimo Wilaya ya Hai Simon Bunda akitoa maelezo wakati wa warsha ya mafunzo ya uhifadhi mlima Kilimanjaro kwa waalimu wamazingira kutoka shule 25 wilayani Hai. |
Afisa mazingira wilaya ya Hai Alfred Njegite akitoa maelezo wakati wa warsha ya mafunzo ya uhifadhi mlima Kilimanjaro kwa waalimu wamazingira kutoka shule 25 wilayani Hai. |
Na Praygod Munisi na Davis Minja
HAI
Imeelezwa
kuwa jamii ya watu wanaoishi karibu na hifadhi ya mlima Kilimanjaro wanao
wajibu mkubwa wa kusaidia kutunza mlima Kilimanjaro ili kuendelea kupata faida
na huduma zitokanazo na mlima huo.
Hayo
yamebainishwa na Afisa maliasili wa Wilaya ya Hai Mbayani Mollel wakati wa
warsha ya mafunzo ya siku moja ya uhifadhi wa mlima Kilimanjaro kwa walimu wa
mazingira kutoka shule 25 za msingi pamoja na waratibu elimu kata.
Amesema
kuwa kwa sasa bado kuna uhitaji mkubwa kwa jamii zilizozunguka mlima huo kuweka
nguvu kwa kushirikiana na klabu za mazingira zilizopo shuleni ili kuweka
msisitizo kwa wanafunzi kuwa na chachu ya kuhifadhi mazingira.
Mollel
ameongeza kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazo kabili uhifadhi wa mazingira
ikiwa ni pamoja na,uvamizi wa misitu kwaajili ya kilimo,kuchoma misitu,kuingiza
mifugo katika hifadhi ya misitu pamoja na ukataji miti kiholela jambo ambalo
limekuwa likitishia hali ya uhifadhi wa mazingira.
Kwa
upande wake Mgeni rasmi katika uzinduzi wa warsha hiyo Kaimu mkurugenzi wa
halmashauri ya Wilaya ya Hai Edward Mtakiliho amepongeza jitihada zinazo
endelea kufanywa na walimu wa mazingira katika shule 25 zinazo zunguka mlima
huo ambazo zimeonesha jitihada chanya za barafu ya mlima kilimanjaro kuongezeka
au kubakia katika hali ya matumaini ya kuongezeka.
Ameongeza
kuwa ikiwa jamii yote pasipo kutegemea uhifadhi huo kufanywa na wanafunzi au
shule hali ya mazingira inaweza kuboreshwa kwa miasi ,ikubwa na kuzidi kuleta
mafanikio zaidi.
Naye
Rais wa Rotary klabu ya machame Raymond Uronu ameitaka serikali kuongeza nguvu
katika makali ya sheria zinazo tumika kusimamia mazingira ili sheria hizo
ziweze kufanya kazi kama ilivyo kusudiwa.
Uharibifu
wa misitu Tanzania kwa mwaka ni Hekta 372,000 ambapo ni uvunaji haramu, moto, uvamizi mipaka,huku
Mahitaji ya ujazo wa miti ni M3 milioni 62.3 na kilichopo ni M3
milioni 42.8 hivyo upungufu ni M3 milioni 19.5 kwa ajili ya
matumizi. Upungufu huu wa mahitaji ni kichocheo cha uvunaji haramu wa misitu na
kusababisha uharibifu wa vyanzo vya maji na upotevu wa misitu na ongezeko la
hewa ukaa.
No comments:
Post a Comment