![]() |
Jengo la Bweni la Wanafunzi kwenye Shule ya Sekondari Harambee katika Wilaya ya Hai |
Na. Riziki Lesuya
HAI
Naibu Waziri
Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda amefurahishwa na kuridhishwa na usimamizi
wa miradi ya maendeleo Wilayani Hai na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji Yohana Sintoo
kwa usimamizi mzuri unaoendana
na thamani ya fedha iliyotumika.
Pia
amewapongeza wananchi kwa kuunga mkono juhudi za serikali kupitia michango ya
fedha na nguvu kazi katika ujenzi wa bweni
kwenye shule hiyo ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Shule
hiyo ujenzi wa bweni hilo umegharimu kiasi cha shilingi 200,386,000/= ambapo
kati ya hizo mchango wa wananchi ni shilingi 181,986,000/= michango
iliyosimamiwa na serikali ya Kijiji na
kuwataka wananchi wengine nchini kuiga mfano huo ili kuisaidia serikali
kufikisha huduma muhimu kwa wananchi na kurahisisha upatikanaji wa maendeleo.
Sambamba na
pongezi hizo Kakunda ameitaka Halmashauri kutumia utaratibu wa ‘force account’
katika utekelezaji wa miradi midogo kwa kuwa uzoefu umeonyesha miradi mingi
iliyofanyika kwa utaratibu huo imekamilika kwa wakati, kwa ubora huku ikipunguza
gharama za utekelezaji wa miradi kwa kuwa mafundi wanaotumika ni mafundi eneo
husika.
“Tumieni
force account na tumieni mafundi wanaopatikana katika maeneo yenu kwani kazi
zao zimekuwa bora kwenye maeneo mengi, mkifanya hivi mtakuwa mmetoa ajira kwa
wananchi wenu lakini pia mtakuwa mmetekeleza miradi yenu kwa gharama nafuu” alisema
Kakunda.
Kakunda pia
amewataka walimu wa shule hiyo kufanya kazi kwa weledi na kufuata taratibu na
sheria kwa kuwafundisha wanafunzi ipasavyo ili kuwawezesha kukua katika maadili
yanayofaa ikiwa ni pamoja na ufaulu wa wanafunzi hao huku akiwahakikishia walimu
kuwa serikali inatambua na kufanyia kazi madeni yao na kwamba hadi kufikia
mwezi juni mwakani serikali itakuwa imelipa asilimia themanini ya madeni
yanayodaiwa.
No comments:
Post a Comment