|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akikagua miradi ya maendeleo katika hospitali ya wilaya ya Hai alipofanya ziara ya kikazi. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Hai Yohana Sintoo. (Picha na Omary Mlekwa)
|
Na. Adrian Lyapembile
HAI
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo
ameipongeza halmashauri ya wilaya ya hai kwa kuendelea kuboresha miundombinu
katika hospitali ya wilaya hiyo itakayofanikisha kutekeleza azma ya serikali
kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wake.