Friday, September 12, 2014

WANANCHI WA NURE WAPATA BARABARA KWA KIWANGO CHA CHANGARAWE INAYOGHARIMU ZAIDI YA MILIONI 15




Wananchi wa Kitongoji cha Nure Kijiji cha Ng'uni katika Kata ya Masama Kati wamenufaika na ujenzi wa barabara uliojengwa kwa kiwango cha changarawe baada ya kupata msaada wa fedha zaidi ya shilingi milini 10 kutoka kwa wanafunzi wa chuo kiku cha Coventry.

 Kukamilika kwa kazi hiyo pia kumechangiwa na nguvu kazi za wananchi pamoja michngo ya fedha kiasi cha shilingi 5,000,000. 

Barabara hiyo inayokadiriwa kuwa na urefu wa km 3 inatarajiwa kwanufaisha zaidi ya wananchi 600 wanaozunguka eneo hilo,lakini pia wananchi mbali mbali wanaotumia barabara hiyo kwa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Hai, Mwandisi  wa Ujenzi  Wilaya ya Hai  Fredy Kweka, amewashukuru wanafunzi hao kwa kujitolewa kusaidia utekelezaji wa miradi mbali  katika Kijiji hicho na kuwaomba wandelee kusaidia miradi mingine kama ujenzi wa maabara katika shule za kata na miundo mbinu ya barabara.

Kwa upande wake kiongozi wa wanafunzi hao ndugu Daniel Paul ameushukuru uongozi wa kijiji hicho kwa ushirikino  waliounyesha  na kuahidi kuendelea kushirikiana na Kijiji hicho katika kusaidia ukamilishaji wa miradi mbali ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya kupitia Mhandisi wa Ujenzi ili kungalia namna watakavyoendelea kusaidia katika ukarabati wa miundo mbinu ya barabara.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nure ndugu Ramphost  Siao ambaye afla fupi ya kukabidhi barabara hiyo ilifanyika katika shule hiyo, alitoa wito  kwa viongozi wa ngazi mbali mbali ndani ya Wilaya ya Hai kutoa elimu na kuhamasisha wananchi juu ya kutambua  umuhimu wa kuchangia  na kuitunza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na wafadhili.

Ndugu Siao amesema  wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano na kuthamini misaada inayotolewa na wafadhili mbali mbali ili kuwapa moyo wa kuendelea kusaidia.

Naye Diwani wa Kata ya Masama Kati ndugu Deogratius Kimaro ameahidi kufuatilia na kuhamasisha wananchi wa kata hiyo kuthamini michango inayotolewa na serikali,wananchi na wafadhili .

Umoja wa wanafunzi hao umekuwa ukisaidia Kijiji hicho kufanikisha miradi  mbali mba ya maendeleo kwa miaka mingi sasa   ikiwa ni pamoja na misaada waliyoitoa  kukamilisha miradi katika shule ya msingi Nure ambapo walitooa shilingi milioni 8 kukamilisha ujenzi wa bwalo,viti 200 vya plastiki.

Katika shule ya sekondari Ng’uni walitoa  vitabu vya sayansi venye thamani ya shilingi  3,500,000 ,walichangia ujenzi wa bwalo kwa shilingi 4,000,000  pamoja tank la maji  lenye thamani ya shilingi 500,000.

Na katika kusaidia wakina mama wa kijiji hicho walitoa  zaidi ya shilingi 25 kusaidia kituo cha usindikaji wa maziwa kwa akina mama wa kijiji hicho.

No comments:

Post a Comment