Akizungmza siku
moja kabla ya mtihani huo kufanyika, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Hai ndugu Melkizedeck Humbe amesema wanafunzi
hao watafanya mtihani hiyo katika vituo
21 ambavyo maandalizi yote yalikuwa
yamekamilika na kupatiwa vifaa vyote.
Ndugu humbe
aliwaagiza wasimamizi wa mitihani katika kusimamia mithani bila ya udanganyifu
katika kusimamia mitihani hiyo na kuwataka kufuata taratibu za utumishi wa
Umma.
Kwa upande
mwingine alitoa wito kwa wanafunzi wa darasa la saba kuondoa hofu na kutokuwa na
wasiwasi wakati wa kufanya mtihani
huo,pia aliwataka wafanye mtihani hiyo kwa hali ya usafi ili kurahisisha
usahishaji wa mitihani.
No comments:
Post a Comment