Monday, June 16, 2014

TAARIFA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA





TAARIFA YA MFUMO WA ULINZI KWA MTOTO PAMOJA NA MAADHISHO WILAYA HAI ILIYOSOMWA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI NDUGU M.O.HUMBEKATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA NA UZINDUZI WA KITUO CHA ONE STOP CENTER


NDUGU  MGENI RASMI ;  Mei  2010  Halmashauri ya Wilaya kwa kushirikiana na Idara ya Ustawi wa Jamii makao makuu  na UNICEF Tanzania, ilifanya utafiti   juu ya ulinzi kwa mtoto matokeo yalikuwa kama ifuatavyo.
      Kiwango cha uelewa wa jamii juu ya ulinzi kwa mtoto ni mdogo sana.
      Mfumo na muundo wa timu ya ulinzi kwa mtoto sio makini katika kupinga na kuitikia  ukatili  dhidi ya  kw a watoto. 
      Idadi kubwa ya makao ya kulea watoto  na mengi kuendeshwa chini ya kiwango .
NDUGU MGENI RASMI; Utafiti huu ulipelekea Wilaya kuwa na mikakati ifuatayo;
      Kuunda timu za ulinzi kwa mtoto
      Kupunguza makao ya kulea watoto yatima na watoto wa mazingira hatarishi
      Kupinga na kuitikia ukatili dhidi ya watoto.

NDUGU  MGENI RASMI;  Baada ya utafiti Halmashauri kwa kushirikiana na wadau  ilibaini kuwa mifumo iliyopo ya haina ushirikiano wa kutosha  katika kutoa huduma kwa watoto  waliofanyiwa ukatili ndipo  mkakati wa uundaji wa  timu ya ulinzi kwa mtoto kuanzia ngazi ya wilaya ,kata na vijiji uliundwa kwa kuzingatia sekta zote zinzazohusika na ulinzi na usalama kwa mtoto wakiwemo,Maafisa ustawi wa jamii ,Mipango ,Hakimu mkazi  (W),Wajumbe kutoka baraza  baraza la watoto, Polisi dawati la jinsia na watoto& mwendesha mashtaka Afisa huduma kwa jamii, Afisa maendeleo ya jamii, Mwanasheria Wilaya  Afisa  Elimu Sekondari ,Afisa elimu msingi  , Madaktari  wawili na Afisa afya Wawakilishi wa wawili wa asasizisizo  za serikali  kutoka ( KIWAKUKI NA HANGO).

NDUGU MGENI RASMI;  Mafanikio yaliyopatikana baada ya kuanzisha mfumo wa ulinzi kwa mtoto
      Kupunguza makao ya watoto kutoka 22 hadi kufikia 7 kwa kufunga  makao na kutoa mwongozo wa kitaifa  ambayo yanaendeshawa chini ya  kiwango ,
      Kuwaunganisha watoto  179  na familia zao/jamii kutoka katika makao   ya watoto yanayolea watoto yatima na mazinhira magumu, watoa huduma 497 wa watoto wamepata mafunzo juu ya ulinzi   na usalama wa mtoto  kisheria. ( walimu 342  ,manesi 40 ,polisi 76 , maafisa wa mahabusi ya watoto, makatibu wa baraza la kata, maafisa magereza  2  and madiwani 2, Mahakimu 8 kutoka Mahakam ya wilaya na mahakama ya mwanzo.
      Walezi( fit person) 50 wa watoto waliofanyiwa ukatili wametambuliwa  katika jamii,
      Kuwepo na mfumo wa ukusanyaji wa taarifa za watoto walio fanyiwa ukatili (child protection informationManagement  system)
      Kuongezeka kuripotiwa kwa matukio ya watoto waliofanyiwa ukatili na watu wazima waliofanyiwa ukatili wa kijinsia  kwa sababu ya kuwepo na uelewa mkubwa katika jamii juu ya kupinga ukatili kwa watoto na unyanyasaji wa kijinsia (Vionlence agaist children (VAC)& Gender based violence (GBV) kutoka 59 mwaka 2009  hadi kufikia  3306 kwa mwaka 2013.
      Kuwepo na ushirikiano mkubwa sana baina ya ofisi ya ustawi wa jamii ,dawati la  na watoto jinsia,mahakama ,elimu, na hospitali, kuwahudumia watoto na wadau wengine
      Watoto kuweza kuripoti matukio ya ukatili  katika dawati la jinsia na watoto polisi na ustawi wa jamii.
      Kesi za watoto kupewa kipaumbele katika mahakama.
      Kutolewa kwa msaada wa dharura kwa watoto waliofanyiwa ukatili 275
      Watoto 330  wa mazingira magumu wamepatiwa vyeti vya kuzaliwa
      Kuwepo na kituo jumuishi cha kutoa  cha kutoa huduma za pamoja kwa watoto waliofanyiwa ukatili pamoja ukatili wa kijinsia (one stop centre) ambacho kinahusisha watoa huduma watatu polisi,daktari na ustawi wa jamii.
NDUGU MGENI RASMI; Changamoto tunazokutana nazo katika kufanya shughuli za ulinzi kwa mtoto.
      Baadhi ya mila na desturi ni kikwazo katika kutoa taarifa za ukatili kwa watoto  kama vile ndoa za mapema
      Kukosa ushirikiano kutoka kwa wanajamii katika utoaji wa ushahidi mahakamani  hususa kesi za ukatili wa kingono (kubaka ,kulawiti na unajisi)

NDUGU MGENI RASMI; Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wadau waliotuwezesha kufika hapo tulipo ,UNICEF Tanzania,Save the children Tanzania,Wizara ya Afya na ustawi wa jamii-  idara ya  ustawi wa jamiii ,wizara ya mambo ya ndani idara ya polisi,wizara ya wanawake  jinsia na watoto na wizara ya katiba na sheria - idara  ya  mahakama  ,pamoja na asasi za kiaraia. NDUGU MGENI RASMI; Makakati wa wilaya katika kupinga ukatili kwa watoto ni;
      Kutoa huduma kwa umakini na weredi katika kituo jumuishi kwa watoto waliofanyiwa ukatili na watu wazima walio fanyiwa ukatili wa kijinsia
      Kuelimisha jamii kwa njia ya radio ,televisheni,shule za sekondari na msingi , taasisi za kidini ,vyama vya kisiasa na mitandao mingine ya kijamii.
      Kuunda timu katika kata 4  mpya na vijiji 5 vipya
      Kuendeleo kuwaunganisha watoto katika jamii kutoka katika makao na wengine walio kitengana na familia au jamii zao.
      Kuendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha mfumo  na muundo wa ulinzi kwa mtoto uliopo.
      Kuwepo na usafiri  wa uhakika katika kuitikia na kufuatilia  matukio  za ukatili kwa watoto
      Kuendelea kutumia fursa zilizopo katika kutekeleza shughuli za ulinzi kwa mtoto.

NDUGU MGENI RASMI; Mwisho tunapenda kutoa wito kwa Wilaya nyingine kuanzisha mfumo huu wa ulinzi na usalama ili kuweza kwa mtoto ili kuweza kumlinda na kumjali mtoto wa Kitanzania.

No comments:

Post a Comment