Tuesday, June 10, 2014

WILAYA YA HAI KUZINDUA KITUO JUMUISHI SIKU YA MTOTO WA AFRIKA


Katika kuhadhimisha siku ya mtoto wa Afrika Wilaya ya Hai inatarajia kuzindua Rasmi kituo Jumuishi  cha kutoa huduma kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa  kijinsia ni kituo cha pekee kwa Tanzania Bara.

Uzinduzi wa kituo hicho kimelenga kurahisisha kupatikana kwa huduma kwa watoto walioathiriwa kijinsia kwa kutoa huduma zote muhimu katika eneo au kituo kimoja.

Akizungumza katika kipindi cha Redio Boma Hai FM  Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Hai Bi Sango Omari amezitaja huduma hizo muhimu kuwa  ni pamoja na huduma zinazotolewa na Ofisi ya Ustawi wa Jamii,huduma zitolewazo na Jeshi la Polisi na Huduma za Kiafya kwakua katika kituo hicho kutakuwa na Afisa Ustawi,Polisi na Daktari kwa ajili ya kuruhisisha kutoa huduma.

Naye koplo John kutoka katika kituo cha Polisi cha Hai amesema kuwepo kwa kituo hicho kwa Wilaya ya Hai ni matokeo mazuri ya utendaji kazi wa Ofisi ya Ustawi wa jamii kwa kushirikiana na  Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia.

Kwa upande wake Afisa Habari  wa Wilaya hiyo bi Riziki Lesuya amewataka wananchi wa Wilaya ya Hai pamoja na maeneo jirani kuhudhuria katika uzinduzi wa kituo hicho ambacho ni cha pili kwa tanzania,kituo cha kwanza kimejengwa Zanzibar.

Afisa Habari amesema kituo hicho kimejengwa kwa ajili ya kusogeza huduma kwa wananchi hivyo ni vema wananchi wakashiriki katika siku ya uzinduzi wa kituo hicho ili waweze kupata elimu juu ya ukatili wa kijinsia kupitia hotuba mbali mbali za  viongozi zitakazotolewa siku hiyo  na vikundi mbali mbali vya burudani.

No comments:

Post a Comment