Tuesday, May 13, 2014

WAUGUZI WILAYANI HAI WAAHIDI KUFANYA KAZI KWA BIDII



Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Hai akiwa ofisini kwake.

 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Hai akitoa zawadi kwa mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo

 Afisa Tawala wa Wilaya ya Hai Bi Julieth Mushi akikabidhi zawadi kwa mmoja wagonjwa aliyelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Hai.







 wauguzuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Hai wakiwa wamewasha mshumaa katika kuadhimisha siku ya wauguzi duniani


 Mwenyekiti wa Chama cha wauguzi Wilayani Hai bi Rehema Antoni Pepin akiwa anatafakari kabla ya kuojiwa na waandishi wa habari

 miongoni mwa wagonjwa walilazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Hai akipokea zawadi wakati wa maadhimsho hayo

 wauguzi wa wakiwa wanatembelea wagonjwa katika kuadhimisha siku ya wauguzi duniani






Wauguzi Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wameazimia kufanya kazi kwa bidii sambamba na utandawazi ili kuendana na kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya wauguzi duniani ambayo ni ‘wauguzi ni nguvu ya mabadiliko na rasilimali muhimu kwa afya’ .

Wauguzi hao walifikia maazimio hayo katika kuadhimisha siku ya wauguzi Wilayani Hai iliyofanyika jana katika hospitali ya Wilaya ya Hai, ambapo maazimio mengine ni pamoja na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano, kuendelea kufanya kazi kwa ubunifu ili kuboresha huduma kwa jamii nzima.

Akisoma risala ya wauguzi hao kwa mgeni rasmi  bi Felicia Ritte alisema pamoja na changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo wamefanikiwa kuongeza kwa idadi ya wauguzi wasajiliwa toka 40 hadi  131 mwaka 2014, kupatikana kwa jengo la upasuaji wa dharura hasa kwa akina mama, wauguzi wengi kupata mafunzo rejea akitolea mfano PMTCT,PITC, ‘Quality improvement in health Services, Human resource for health for management skilis, professional ethics in health, family palinning, option B+ na infant feeding,’ na baadhi ya wauguzi kupata nafasi ya  kujiendeleza kielimu.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Hai ndugu Nyakaraita Mwita  amewataka wauguzi kufanya kazi kwa weledi na kufuata sheria, taratibu na kanuni za kazi  akisisitiza wauguzi kuwa na huruma kwani kazi hiyo imethaminiwa na jamii na serikali pia.

 ‘uguuzi umethaminiwa , mnahitaji kukidhi kigezo cha kuwa na huruma kwakuwa kazi yenu inahitaji huruma ,muache matumizi ya lugha chafu kwa wagonjwa  na muwajali wagonjwa na kuwapenda’alisema nyakaraita.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Hai ndugu Paul Chaote amesema serikali imekuwa ikishughulikiwa tatizo la uhaba wa wauguzi ambapo kila mwaka imekuwa ikiajiri wauguzi na kwamba mpaka sasa bado Hospitali ya wilaya imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa wauguzi  kwa asilimia 37.

Amesema licha ya upungufu huo wamekuwa wakifanya kazi kwa kujituma na kwamba juhuudi hizo na ushirikiano wa watumishi wote wa Hospitali hiyo imeifanya Hospitali hiyo kushika nafasi ya nne kitaifa katika hudma ya utoaji chanjo.

1 comment: