Hayo yamelezwa na Diwani Kata wa Masama Rundugai Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro , Mh Fadhili Juma wakati akiwsilisha taarifa ya hali ya
utekeleza wa miradi ya kimaendeleo katika kikao
cha baraza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya
Hai
Amesema mabadailiko
ya tabia nchi yaliyotokea yamepelekea
uchumi wa wananchi kuyumba kutokana na kutopata mavuno ya kutosha katika msimu uliopita hali iliyosababisha
wananchi wengi kukumbwa na nja na kushindwa kutoa michango kwani kata hiyo
wananchi wengi hutegemea Kilimo
Kwa upande wake Mh Diwani wa Kata ya Machame Weruweru, Mh Adris
Mandrai akitoa taarifa ya hali ya
utekezaji wa robo ya tatu alisema kuwa miradi inayotekelezwa katika Kata hiyo imeendelea vizuri ila michango ya wananchi imekuwa ya kususua jambo ambalo
limesababisha miradi kukwama.
Alisema mabadiliko ya tabia nchini imepelekea baadhi ya maeneo ya Kata hiyo kuwa katika
hatari ya kukumbwa na baa la njaa endapo mvua za masika zitaisha mapema.
Mh Mandrai amesema kuwa vijiji vilivyopo katika hatari ya
kukumbwa na baa la njaa ni vijiji vya Ngosero na Minjongweni ambapo amefafanua
kuwa pamoja na jamii wananchi kulima kwa
wingi bado tatizo la mabadiliko ya tabia nchi yamendelea kuathiri kutokana na
kukoseka kwa mvua za masika.
Naye Diwani wa Kata ya Masama Kati, mh Deogratus Kimaro
akiwasilisha taarifa katika kikao cha baraza hilo amesema kuwa baadhi ya viongozi wa vijiji wamekwamisha
miradi ya kimaendeleo kutokana na kushindwa
kuitisha vikao vya kisheria .
Kufuati hali hiyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai,Mh Clement Kwayu aliagiza
watendaji wa vijiji ambao wameshindwa kusoma mapato na matumizi kwa muda mrefu
kuandaa taarifa hizo na kuzifikisha katika Ofisi ya Mkurugrnzi mapema wiki ijayo na baada ya hapo waitishe vikao na kutaka kwa atakayeshindwa kutekeleza agizo hilo achukuliwe hatua za kinidhamu.
Kufuatia hilo Baraza la Madiwani pia limewataka wataalamu kutembelea
vijiji ambavyo vimekuwa na migogoro ili kuweza kutatua matatizo ambayo yamekuwa
yakikwamisha kuendelea kwa shughuli za kimaendeleo katika jamii .
Akichangia katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya hiyo, Novatus
Makunga amemtaka Mkurugenzi Mtendaji
kuwachukulia hatua ya kinidhamu watumishi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao jambo
ambalo ni changamoto katika kuteleza shughuli za kimaendeleo
Mh Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai na Diwani wa kata ya Kata ya Machame Kaskazini Clement Kwayu akiwasilisha taarifa ya Robo ya tatu ya kata yake.
Diwani wa kata ya Masama Kusini aliyesimama wakwanza kulia Mh Issa Kiasnga akitoa taarifa ya robo ya tatu ya kata yake,alisisitiza juu ya matumizi ya dawa ya kulevya yanavyoathiri nguvu kazi na kuliomba Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi kuziba mianya ya usafirishaji wa madawa hayo hasa mirungi na bangi ambayo amesema katika Wilaya ya Hai hakuna eneo linalolima madawa hayo ya kulevya yalikini yamekuwa yakitumia na baadhi ya Vijana.
Aliyesimama wa kwanza kulia ni Diwani wa kata ya Machame Mashariki Mh Rajabu Nkya akitoa taarifa ya kata yake 'ninaona fahari kwa kata yangu kuwa na Kaya nyingi zilizojiunga na Mfuko wa Bima wa Afya ya Jamii bado tunaendelea kuhamasisha wananchi wajiunge na mfuko huo.'
Aliyesimama wa kwanza kulia ni Diwani wa kata ya Masama Kati Mh Deogratius Kimaro akitoa taarifa ya robo ya tatu ya Kata yake,'tupo katika mchakato wa kuboresha vituo vya afya na zahanati ili kufikisha huduma kwa wananchi kwa gharama ndogo'
Aliyesimama ni Diwani wa Kata ya Machame weruweru Mh Adris Mandrai akitoa taarifa katika Baraza la Halmashauri mapema jana "mikakati tuliyonayo katika kukamilisha miradi ya maendeleo ni pamoja na kutoanzisha miradi mipya kabla ya kukamilisha iliyopo,kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwa wananchi na kuhamasisha uchangiaji miradi ya maendeleo'
Mh Fadhili Mchomvu Diwani wa Masama Rundugai akitoa taarifa ya Robo tatu ya Kata yake.
Diwani wa kata ya Machame Kusini Mh Nasibu Mndeme akitoa taarifa ya robo ya tatu ya kata yake,"tunaendelea kuzuia utengenezaji wa pombe kwakutumia mahindi na kuzingatia kilimo bora ili kuepukana na uhaba wa chakula"
No comments:
Post a Comment