Mkuu huyo wa Wilaya ametoa agizo
hilo baada ya kukagua barabara hiyo ambayo ilikarabatiwa kwa kipande cha
kilometa 7.9 na Wakala wa barabara nchini, Tanroads na baadaye alikagua
barabara nyingine ya Kwasadala hadi Masama inayoendelea kujengwa na wakala huyo.
Akizungumza na viongozi mbalimbali
wa vijiji vya kata ya Machame Kaskazini ambapo barabara hiyo imepita,aliwaiwaagiza
Watendaji hao kusimamia sheria inayozuia mifugo kutembezwa barabarani badala ya
wao kama viongozi kuanza kulalamika.
Viongozi hao awali walimweleza Mkuu
huyo wa Wilaya kwamba kwa asili ya eneo la Machame siyo la ufugaji wa mifugo
inayochungwa bali ufugaji wao ni ule wa ndani, hata hivyo limezuka wimbi la
wamiliki wa Mabucha kwenda minadani na kununua ng’ombe ambao katika kuwasafirisha
uamua kuwachunga barabarani na hivyo kusababisha uharibifu wa barabara.
Kwa upande mwingine Makunga
amemwagiza Kaimu meneja wa Wakala wa Barabara, Tanroads Mkoani Kilimanjaro
Mhandisi Reginald Massawe kuandaa semina ya uelewa kwa viongozi wa vjiji na
vitongoji itakayolenga kuwaelimisha juu ya sheria ya hifadhi ya barabara pamoja
na mpango wa kuisimamia na kuwapa nakala ya sheria hiyo ili waanze kuitekeleza.
Pia amewataka viongozi hao kutoa
notisi kwa wamiliki wa mabucha kuhusiana na kuanza utekelezaji wa sheria hiyo.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya
amemtaka Mhandisi Massawe kutuma wataalamu watakaoianisha mapungufu mbalimbali
ambayo yamejitokza katika ukarabati huo wa baabara yakiwemo ya baadhi ya maeneo
kutokuwa na makalvati, mikondo ya maji kutokuelekezwa kwa usahihi, baadhi ya
maeneo ya lami kuanza kumeguka pamoja na
mahitaji ya kuweka alama za kuvuka kwa waenda kwa miguu.
Awali mhandsi Massawe ameeleza
wakala wa barabara imetumia kiasi cha shilingi milioni 1,005 kukarabati sehemu
ya kilometa 7.95 ya barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 14.98.Amesema kazi
zilizofanyika ni pamoja na kuondoa tabaka la lami, kuvuruga msingi wa awali, kujenga
msingi mpya nakuweka tabaka jipya la lami nyepesi kwa upana wa barabara wa mita
9.0.
Amesema kuwa dosari mbalimbali
zilzojitokeza ambazo walizibaini katika ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ambazo
znahtaji fedha nyingi zitafanyiwa kazi katika awamu ijayo ya kukarabati
barabara hiyo ambayo itaingizwa katika mwaka ujao wa fedha ambao unaanza mwezi.
Amesema kuwa katika mwaka ujao wa
fedha kiasi cha shilingi milioni 800 zimetengwa kwa kazi ya kupanua mabega ya
barabara kila upande na kujenga tabaka la lami nyepesi sehemu ya barabara yenye
urefu wa kilometa 5
Akiwa katika barabara ya
Kwasadala hadi Masama mkuu huyo wa wilaya amemtaka Mkandarasi kushirikiana na
viongozi wa eneo hilo katika kuhakikisha ujenzi wa makalvati ya kupitisha maji
unakwenda kwa usahihi kwa lengo la kuepuesha madhara hasa nyakati za masika.
Aidha amemtaka Mkandarasi huyo
kutatua tatizo la baadhi ya maeneo kushindwa kupitika kutokana mvua zinazonyesha
sasa kwa kumwaga vifusi hasa katika maeneo yenye miteremko mikali.
Mkandarasi mpya wa barabara hiyo
kampuni ya Hari Singh and Sons Limited ameahidi kurekebisha sehemu zote korofi
katika kipindi hiki cha mvua wakati kazi ya ujenzi huo ambayo imefikia asilimi
tano ikiwa inaendelea.
Mkandarasi huyo alianza kazi mwezi
Januari mwaka huu baada ya kuvunjwa kwa mkataba wa Mkandarasi wa awali katika
barabara hiyo ambayo ni ahadi ya rais Jakaya Kikwete.
Ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu
wa Kilometa 12.5 unatarajiwa kukamilika mwezi Januari Mwakani.
Mkuu
wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akipata ufafanuzi wa Ujenzi wa Barabara ya
Machame kutoka kwa Kaimu Meneja wa Tanroads mkoani Kilimanjaro, Mhandisi
Reginald Massawe(Kushoto)
Mwenyekiti
wa kijiji cha Nshara akimwonyesha mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga pamoja
na Maofisa wa Tanroads mkoani Kilimanjaro moja ya eneo hatari kwa watumia barabara
ya Machame katika kona ya Lambo
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga na maofisa wa Tanroads
wakishuhudia mifugo ikisagwa katika barabara ya Machame
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akitoa maelekezo ya
barabara ya Machame,kulia ni mmoja ya wataalamu wa ujenzi katika wilaya ya
Hai,Mhandisi Peace
Mkuu wa wilaya ya Hai akiangalia moja ya eneo la barabara ya
Machame ambalo lina kasoro katika ukarabati wake huku maofisa wa Tanroads mkoa
wa Kilimanjaro wakitoa maelezo




No comments:
Post a Comment