Monday, May 26, 2014

HOTUBA YA MKUU WA WILAYA YA HAI NDUGU NOVATUS MAKUNGA AKIFUNGA MAFUNZO YA USAFI WA MAZINGIRA YALIYOFANYIKA HIVI KARIBUNI KATIKA UKUMBI WA HALMSHAURI YA WILAYA



HUTUBA YA MKUU WA WILAYA YA HAI, NOVATUS MAKUNGA YA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA UTAMBUZI WA USAFI NA MAZINGIRA SHULENI  KWA WILAYA YA HAI MNAMO  MEI 16,2014
.Makamu mwenyekiti wa halmashauri
.Waheshimiwa madiwani
.Wawakilishi wa vyama vya siasa
.Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya,
.Wakuu wa idara,
.Mabibi na mabwana,

Awali ya yote nianze kuwashuru wote mlioshiriki katika kufanikisha mafunzo haya yanayolenga kuileza jamii umuhimu wa usafi wa mazingira mashuleni ili kupunguza maradhi mengi yanayosababisha vifo kupitia uchafu.

Tayari muongozo wa usimamizi wa mkakati huu umeshatengenezwa lakini lengo ni kuwajenga watoto hususani wanafunzi ambao watawezesha familia zilizopo na zijazo zinaepukana na uchafu wa mazingira.

Mkakati huu katika kuanza umelenga kuwa na  vyoo bora na matumizi yake pamoja na miundombinu ya kushughulikia takataka zinazozalishwa katika shule zetu.

Hadi kufikia hatua hii ya mafunzo ya utambulisho wa mpango huu,tayari baadhi ya kazi zimeshafanyika ikiwemo ya kutengeneza muongozo.

Katika kutengeneza muongozo huo nina imani maeneo mbalimbali yamezingatiwa yakiwemo kutoa elimu kwa wadau mbalimbali,kukusanya takwimu za awali,uhamasishaji,kufanya zoezi la uchefuaji katika jamii na ufuatiliaji wa karibu.

Ndugu wana mafunzo, katika mpango huu wa usafi ya mazingira nimebaini kwamba eneo la kwanza mnaloanza nalo ni matumizi sahihi ya vyoo ambapo ujenzi wake utazingatia miongozo iliyotolewa na wizara.

Niwashukuru wenzetu wa UNICEF kwa kutoa msaada wa kujenga vyoo bora vitakavyozingatia miongozo mbalimbali ikiwemo ya mahitaji ya walemavu na sehemu ya kujihifadhi wasichana wakati wa siku zao za mwezi.

Usimamizi mbovu wa mazingira  hasa kutokutumia vyoo ama matumizi ya vyoo visivyokuwa na ubora na hatimaye idadi kubwa ya wanafunzi kujisaidia hovyo,athali zake ni kubwa kwani husababisha jamii kuendelea kurisishana tabia hiyo husababisha mfumo usiokwisha wa kuenea kwa magonjwa.

Ndugu wana mafunzo,maradhi ni mojawapo wa maadui watatu ukiacha ujinga na umaskini ambao serikali imekuwa ikipigana nao tangu Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961.

Kuwepo kwa Mkakati wa Matumizi ya vyoo sahihi katika shule unaweza kuwastua wengi lakini hatuna budi kuutekeleza ili kuhakikisha kwamba tunakuwa na jamii bora ambayo haikwazwi na changamoto ambazo zipo ndani ya uwezo wetu zikiwemo za maradhi.

Ndugu wana mafunzo, mimi nipongeze hatua hii kwani unaweza kuangalia mambo kwa ujumla na ukadhani  yanakwenda vizuri lakini ukajikuta umejisahau katika eneo moja ambalo ni nyeti sana nalo ni la usafi wa mazingira.

Eneo la huduma za vyoo ni eneo muhimu sana kwa maisha bora ya mtu ingawa tunaweza kujiona tupo nyuma sana.

Wanasaikolojia wanabainisha kwamba vyoo vinapokuwa duni,uchangia kudumaza maendeleo ya sekta ya elimu kwa sababu wanafunzi wenye matatizo ya kuhara ama kwa mfano mwanafunzi msichana aliyeko katika hedhi hushindwa kwenda shule kwa kuwa hakuna mazingira rafiki ya kujistiri.

Utafiti wa shirika la Water Aid linalofanya shughuli zake katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania inaonyesha kuwa hali ya vyoo katika nchi za Afrika mashariki ikiwemo Tanzania inasikitisha huku watoto wa kike wakielezwa kuathirika zaidi kutokana na maumbile yao kuhitaji usafi.

Mkataba wa Dakar wa elimu kwa wote unataka ifikapo mwaka 2015,watoto wote wawe wana uwezo wa kupata elimu ya msingi iliyo bora ikiwemo na uhakika wa huduma za vyoo na mazingira ya shule kwa ujumla

mafunzo,mpango huu umekuja wakati muafaka ambapo tatizo la vyoo bora katika shule zetu linaeeza kuwa ni hali halisi inayoakisi tatizo lililopo katika jamii yetu.

Katika wilaya ya Hai katika utafiti uliofanyika mwaka jana umebaini kwamba kati ya kaya 7,398 zilizopitiwa imebainika kaya 1,479 hazikuwa na vyoo kabisa.

Namba hii ni kubwa na si namba ya kubeza ukiondoa idadi nyingine kubwa tu ya kaya ambavyo zilikuwa na vyoo vya asili.

Ndugu wana mafunzo katika kuibadili jamii yetu basi nguvu kubwa tuelekeze katika kuboresha upatikanaji wa vyoo bora mashuleni hali ambayo mwisho wa siku itaeneo mpaka katika nyumba zetu tunazoishi.

Eneo la pili ambalo mnatarajia kuanza kwa msaada wa wenzetu wa UNICEF ni pamoja  na ujenzi wa miundombinu ya kuchomea sodo zilizotumiwa na wanafunzi yaani incenerator.

Eneo hilo nalo lina changamoto kubwa sana kwa idadi kubwa ya shule zetu kutupa taka hovyo kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu ya kuzishughulikia taka zinazozalishwa.

Changamo hiyo inaenda mpaka katika ngazi ya Halmashauri yetu ambayo mpaka sasa haijawa na mfumo mzuri wa udhibiti wa taka ingawa hivi sasa ipo mbioni kubuni mkakati wa urejezaji wa taka ambao ndiyo wa kisasa zaidi na unaotumika mpaka katika nchi

Ndugu wadau,katika zoezi hili la usafi wa mazingira ambalo tunaanza na vyoo bora na takataka zinazozalishwa shuleni pia ningependa kutoa msisitizo wa elimu ya umuhimu wa kunawa mikono.Kunawa mikono ni eneo la muhimu sana.Tunaelezwa na tumekuwa tukikumbushwa umuhimu wa kunawa mikono na sasa tunaingia katika kampeni ya kuwa na vyoo bora.

Naamini hakuna asiyefahamu umuhimu na wakati muafaka wa kunawa mikono ambapo  ni pamoja kabla ya kushika chakula,baada ya kutumia au kutoka chooni.

Katika suala la kunawa mikono jamii kubwa hawalizunguzi na linapozungumziwa jamii nyingi hazifuati taratibu za kunawa mikono na badala yake wengi hutumia maji ambayo si salama kunawa mikono.

Katika kutengeneza muongozo wa utekelezaji,mmebainisha kuwa mmelenga kusaidia utekelezaji wa sera mbalimbali za kitaifa.

Katika jitihada za kuhakikisha suala la usafi wa mazingira linafanikiwa serikali imekuwa na sera mbalimbali za kitaifa ambazo ni pamoja na dira ya taifa ya maendeleo 2025 ambapo lengo kuu la dira hiyo ni kuboresha maisha ya mtanzania kwa kuboresha afya ya msingi,afya ya uzazi,kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto,kuongeza umri wa kuishi,upatikanaji wa maji safi na salama kwa wote,uhakika wa chakula cha kutosha na salama,kufikia lengo la usawa wa kijinsia katika ngazi mbalimbali za maamuzi ya kiafya na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika mipango ya utoaji wa huduma za afya.

Aidha sera hizo zinabainishwa kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii ambapo kuna  mpango wa maendeleo ya afya ya msingi,mmam wa mwaka 2007 hadi 2017.

Baadhi ya malengo ya mpango huu ni kuboresha afya ya mazingira kuanzia ngazi ya kaya,kuwajengea uwezo maofisa mazingira katika ngazi ya wilaya na kata wa jinsi ya kuhifadhi mazingira,kuelimisha na kushirikisha jamii katika kufuata kanuni na taratibu za usafi katika kanuni za kutunza mazingira.

Ndugu wana mafunzo,pamoja na uzinduzi huu,lakini katika kufanikisha zoezi zima naagizo yafuatayo;
1.Ni lazima kuwepo na mkakati wa asilimia mia moja kutekeleza kwa kumaanisha kama mlivyobainisha katika risala yenu ya ushirikishwaji wa jamii ya shule,wazazi,walimu,kamati za shule na wanafunzi.
2.Tutengeneze mfumo wa ufuatiliaji wa miundombinu ya vyoo na udhibiti wa taka katika shule na ikiwezekana tuwe na mashindano ya usafi.

Ndugu wana mafunzo na sasa natangaza rasmi nimeyafungua mafunzo ya utambulisho wa usafi wa mazingira mashuleni.

AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA

1 comment: