Bodi ya Afya Mpya ya Afya
Wilayani humu imetakiwa kusimamia kamati zote zilizoko chini yake na kuhakikisha
kuwa huduma za Afya katika Wilaya yetu
zitaboreshwa katika viwango vinavyopendekezwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii.
Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Mganga Mkuu
wa Wilaya ya Hai Dr Paul Chaote wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo katika
Mkutano wa Bodi hiyo ulio ambatana na uchaguzi wa Mwenyekiti Mpya wa kuongoza Bodi hiyo ambapo
Bw Inocavity Swai alichaguliwa
kuwa Mwenyekiti.
Amesema kuwa Bodi ya afya ya Wilaya inayomaliza kipindi chake ilisimikwa na kuanza kazi rasmi mwezi oktoba mwaka 2010 lengo ikiwa ni kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu lakini kutokana na kuchelewa mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wapya,Bodi hii iliendelea kuwapo madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi. Aliongeza kuwa Katika kipindi cha miaka minne bodi kwa kushirikiana na timu ya uendeshaji shughuli za afya pamoja na Menejimenti ya Halmashauri ilifanya mambo mbalimbali ikiwamo Kuongeza wigo wa huduma katika hosipitali ya wilaya kwa kufanya upanuzi kutoka majengo 7 mwaka 2010 hadi majengo 11 mwaka 2014. Chaote aliongeza kuwa mambo mengine ni pamoja na Kufanya ukarabati katika vituo vya Afya na Zahanati,Kuongeza vituo vya hiduma toka 60hadi 62,Kufanya ziara elekezi za usimamizi katika hosipitali ya Wilaya nay a Machame,Vituo vya Afya na Zahanati na Kuingia mikataba 3 ya kiushirikiano kuendesha vituo vya makanisa ikiwa ni pamoja na hosipitali teule ya Machame. “Pia tumeweza ku Kufanya uhamasishaji wa mfuko wa afya ya jamii katika mikutano ya wananchi,mikusanyiko ya watu kama masokoni,makanisani na misikitini,katika shule za sekondari na kuongeza wanachama kutoka kaya 854 mwaka 2010 hadi kaya 5,028 mwaka 2014,Kufungua akaunti katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali.”alisema Dr Chaote "Ni jambo la kunivunia kuona kuwa licha ya changamoto nyingi zinazo jitokeza ndani ya hosipitali yetu na vituo vingine fya Afya bado Bodi ya Afya imeweza kutoa huduma kwa wananchi pamoja na kuwaelimisha kuhusu bima za afya ili kila kaya iweze kupokea matibabu yaliyo bora kpitia bima ya Afya."Alisisitiza Chaote. Alisema kuwa mbali na mafanikio hayo yote pia wameweza kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo uchangiaji mdogo wa wananchi katika masuala ya mfuko wa afya ya Jamii ambapo lengo la kitaifa ifikapo disemba 2015 ni 30% wakati wilayaya Hai bado ni 10%tu,uchakavu wa majengo katika baadhi ya vituo,ukosefu wa huduma za maabara katika zahanati za Serikali ukosefu wa baadhi ya huduma muhimu katika Hosipitali ya Wilaya kama nishati mbadala wakati umeme wa Tanesco unapo katika. |
No comments:
Post a Comment