Kamati ya Maafa Wilaya ya Hai ikiongozwa na Mkuu
waa Wilaya ya Hai Antony Mtakahivi karibuni imetembelea maeneo yaliyoathiriwa na mvua iliyosababisha
Kaya 50 kukosa sehemu za kuishi katikabaadhi ya vijiji vya Kata ya Weruweru ,Masama Rundugai na Mnadani
ili kujionea hali halisi huku wakiwapa pole na kuwataka viongozi wa vijiji
husika kufanya tathimini haraka iwezekanavyo ili wananchi hao kuweza kusaidiwa
kwa namna yeyote ile.
Mtaka aliwataka wananchi kusaidina bila ya
kujali itikadi za siasa na kusisitiza juu ya wale walioathirika kupatiwa
hifadhi.
“Niwaombe wale ambao hawaja kumbwa na
mafurikom haya kuwa na utu wa kibinadamu kwa kuwapa hifadhi wenzao ili kutoa
nafasi kwa Serikali kutafuta misaada mingine inayo hitajika”Alisema Mtaka.
Mku wa Wilaya pia aliwataka wananvhi kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki kigumu huku wananchi hao wakitakiwa kufanya
usafi katika maeneo yaliyo athirika ili kuepuka magonjwa ya milipuko.
“zingatieni usafi katika maeneo yenu
kama mnavyo jua ya kuwa mvua hiyo imeharibu vyoo vyenu hivyo ni rahisi kwa
magonjwa ya mlipuko kuwapata msipo fanya usafi ikiwa ni pamoja na kulala katika
vyandarua katika hifadhi mtakazo pata”Alisema Mtaka.
“Ilikuwa ni usiku kama wa saa nane mvua
ilipo zidi na maji kuanza kuingia ndani ya nyumba zetu nilijitahidi kutoka na
mke wangu pamoja na watoto wangu kwani hapa nipo na familia ya watoto kumi kila
kitu kimeharibika na sikuweza kutoka hata na kitu chochote”Alielezea mmoja wa waathirika
wa mafuriko hayo.
Baadhi wa wana vijiji hao wamedai kuwa tukio
kama hilo liliwahi kutokea mwaka 1965 ambapo lilifanya uharibifu kama huo huku
mashine ya kusaga na kukoboa nafaka wakati huo ikichukuliwa na maji.”Walisema
wanavijiji hao.
Tayari watu ambao nyumba zao ziliharibiwa na
mvua wamekwishapata hifadhi kwa majirani zao, huku kilio chao kikubwa kikiwa ni
chakula na mahitaji mengine muhimu ambayo ni pamoja na Nguo na wakati huo huo
wakiwa hawajui waelekee wapi mara baada ya kuharibika kwa nyumba zao.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya amewaomba
wadau na taasisi mbali mbali kutoa
misaada ya chakula,mavazi,dawa na mahitaji mengine muhimu ili kuwasaidia
wananchi hao.
Halmashauri kwa msaada wa dharura ilitoa
maharage kg 302,unga kg 1510,sukari kg 302,chumvi pakti 302,madaftari 100,net
200 na kalam 150 huku baadhi ya watumishi na wananchi mbali mbali wakitoa nguo
kwa ajili ya kuwasaidia walioathirika na mafuriko hayo.
No comments:
Post a Comment