Mkuu wa Wilaya ya Hai ndugu Novatus Makunga amewataka wananchi kutambua umuhimu wa mazingira ili kujinusuru na athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira.
Mkuu wa Wilaya
ameyasema hayo wakati wa hafla ya
kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la uhifadhi wa mazingira kupitia Mradi
wa matumizi endelevu ya ardhi(SLM), na kufanyika katika ukumbi wa Halmashauri
hiyo na kuwashirikisha wadau mbali mbali wa mazingira.
Makunga
amezitaja athari mbali mbali zinazotokana na uharibifu wa mazingira kuwa ni
pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa unosababisha uzalishaji duni wa mazao ya
chakula na bisahara lakini pia ongezeko la joto katika maeneo mbali mbali
duniani.
Kufuatia hali
hiyo amewataka wananchi kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti na kuitunza miti
hiyo ikiwa ni njia moja wapo ya kurejesha hali ambayo kwa sasa imetoweka kwa
muda mrefu.
Amewatakwa
washindi hao kuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha wananchi kutunza mazingira
kwa kuotesha miti rafiki katika vyanzo vya maji na maeneo mbali mbali ikiwa ni
pamoja na maeneo ya makazi,taasisi mbali mbali kama shule,kanisa,misikiti na
viwanda.
Kwa upande
mwingine amewataka wanachi hao kutumia vema mafunzo waliyoyapata ya ufugaji wa
nyuki ili kuwaongezea kipato cha kaya na kukuza uchumi wa wilaya ya Hai na nchi
kwa ujumla.
Amesema
kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababisha uzalishaji wa kahawa
kupungua katika maeneo mengi ya Mkoa wa Kilimanjaro,zao ambalo lilikuwa ni
tegemeo la kipato kwa wananchi wengi,ni vema wakabali mtazamo huo na kufuga
nyuki kama chanzo mbadala cha uchumi.
Awali akisoma taarifa
ya utekelezaji wa mradi huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai
ndugu Melkizedeck Humbe amesema mradio huo unatekelezwa katika bonde la mto Kikafu.
Amesema mradi
huo wa matumizi endelevu ya ardhi(SLM) kwa Wilayab ya hai yamesaidia katika
kuwapatia wananchi mafunzo mbali mbali ya matumizi sahihi na endelevu ya ardhi
pamoja na ufugaji wa nyuki.
Kwa niaba ya
washindi wa shindano hilo mshindi wa
kwanza wa kikundi cha sifa kilichopata kiasi cha shilingi laki saba ndugu Dominik
Mmasy ameishukuru na kuipongeza serikali kwa kutambua mchango wa wananchi wa
kawaida katika kutunza mazingira na kuomba Halmashauri iendelee na utaratibu
huo ili kuwajengea hamasa wananchi wengine kutunza mazingira.
Katika
mashindano hayo,mshindi wa kwanza kwa
upandi vikundi alizawadiwa kiasi cha shilingi laki saba,kikundi cha pili laki
sita na cha tatu laki tano huku kwa mshindi mmoja mmoja mshindi wa kwanza
alizawadiwa kiasi cha shilingi laki tano,wa pili taki nne na wa tatu laki tatu
pamoja fedha hizo pia washindi wote walitunukiwa vyeti vya ushindi.
Baadhi ya Wakuu wa Idara pamoja wa wadau wa mazingira wakimsikiliza Mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai
Baadhi ya Wakuu wa Idara pamoja wa wadau wa mazingira wakimsikiliza Mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai
Mjumbe wa Timu ya utekelezaji wa mradi wa SLM ndugu Mathew Ntigigwa akiwatambulisha wageni mbali mbali waliohudhuria hafla hiyo,wa kwanza kushoto kwake ni Mratibu wa Mradi wa SLM Wilaya ya Hai ndugu Robert Mwanga.
picha hiyo hapo juu na pamoja na picha sita zinazofuata chini yake ni washindi wa vikundi na binafsi wakikabidhiwa cheti pamoja na hundi.
Mkuu wa Wilaya ya Hai ndugu Novatus Makunga (aliyesimama) akihutubia wadau mbali mbali wa utunzaji wa mazingira Wilayani Hai.(hawapo kwenye picha)
Mmoja wa washindi akishukuru kwa niaba ya washindi wote.
No comments:
Post a Comment