Wednesday, June 25, 2014

AFISA MKUU WA UHAMIAJI MKOA WA KILIMANJARO AMEWATAKA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA WAHAMIAJI HARAMU


Wananchi pamoja na viongozi wa ngazi zote wametakiwa kutoa taarifa wanapomtilia mashaka mtu yoyote kama ni mhamiaji haramu na kuwafichua wote wanaowahifadhi wahamiaji hao  ili  kulinda amani na usalama wa wananchi.

Rai hiyo imetolewa  Afisa  Mkuu wa uhamiaji  Mkoa wa Kilimanjaro ndugu Johanes Msumule wakati wa kuwasilisha mada katika  kikao cha baraza la biashara Wilaya ya Hai ambacho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wa biashara pamoja na wakuu wa idara.

Msumule amesema kuwa  elimu zaidi inaendelea kutolewa kwa wananchi kwani wengi wao wamejikuta wakitahifishiwa mali zao  au kutumikia adhabu mbali mbali pale ambapo wanawafadhili au kuwahifadhi wahamiaji haramu kitendo ambacho ni kinyume na sheria.

Naye Afisa Habari wa Wilaya ya Hai Bi. Rizik Lesuya  ameushauri uongozi wa idara ya uhamiaji kutumia vyombo vya habari kama vile radio, Tv pamoja na magazeti  ili kutoa  elimu hiyo kwa wananchi wengi zaidi .

Naye  Janesta Urio kutoka kutoka sido Kilimanjaro amesema kuwa ili kutoa mwanya zaidi kwa wananchi kutoa taarifa juu ya matukio ya uhalifu viongozi hawana budi kufuata maadili ya kazi yao ikiwemo kumwifadhi mtoa taarifa ili asidhurike kwa namna yeyote ile pale anapotoa taarifa juu ya vitendo vya uhalifu.

Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Hai ndugu Zabriel Moshi amewashukuru washiriki wa kikao hicho sambamba na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizoelekezwa katika ofisi yake likiwemo suala la ukarabati wa choo cha soko la walaji Hai mjini

habari hii imeandikwa
Na Edwin Lamtey

No comments:

Post a Comment