Tuesday, April 29, 2014

HAI YAFANYA VIZURI KWA KUTOA CHANJO-YAKABIDHIWA ZAWADI NA MAMA SALMA



Halmashauri ya Wilaya ya Hai imeshika nafasi ya nne kati ya Halmashauri zote nchini kwakutoa huduma ya chanjo kikamilifu katika siku ya maadhimisho ya chanjo duniani huku Mkoa wa Kilimanjaro ukishika nafasi ya tatu.

Kutokana na hatua hiyo Halmashauri ilikabidhiwa ngao ya Ushindi na Kiasi cha shilingi milioni tano ikiwa ni motisha kwa Halmashauri ya Wilaya ya Hai kuendelea kufanya vizuri na Halmashauri zingine kujifunza kutoka Hai.

Akikabidhi zawadi hizo mama Salama Kikwete  amewataka wazazi, walezi na waalimu kushirikiana katika kuhakikisha kuwa watoto wa kike wenye umri wa miaka tisa hadi kumi na tatu wanapata chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi.

Uzinduzi huo wa chanjo  hiyo ya majaribio ya shingo ya uzazi ulihudhuriwa na Naibu waziri wa afya na ustawi wajamii Dk Kyebwe Stivine Kyebwe, Dk Sudha Sharma mwakilishi toka UNICEF, Rufaro Chatora Mwakilishi toka shirika la afya duniani WHO pamoja na viongozi wengine wakiserikali.

Mke wa raisi amewataka wazazi na walenzi kuondokana na kasumba mbaya ya kusema kuwa chanjo hiyo itawafanya watoto kuwa  wagumba na kusema kuwa chanjo hiyo ni salama kiafya nchi za wenzetu wameweza kutokomeza saratani kwa chanjo ya HPV.



No comments:

Post a Comment