Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga akipokea msaada wa unga wa mahindi kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya Bonite
Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga amewaomba wadau mbali mbali kuendelea kusaidia wananchi wa Wilaya ya Hai waliokumbwa na maafa yaliyosababishwa na upepo mkali ulioambatana na mvua na kuezua paa za kaya zaidi ya 200.
Mkuu wa wilaya alitoa wito huo wakati akipokea msaada wa kilo 2500 za unga wa mahindi, kilo 1000 za maharage na mabati 200 zilizotolewa na mwenyekiti wa makampuni ya IPP kupitia kampuni ya vinywaji baridi ya Bonite Bottlers ya Mjini Moshi.
Alisema miisaada bado inahitajika zaidi kwa
walioathirika hasa kwakuwa wananchi wameanza matayarisho ya kilimo kutokana na
mvua ambazo zimeanza kunyesha na kusisitiza umuhimu wa misaada ya kibinadamu.
Ametaja wadau wengine waliotoa misaada kuwa ni pamoja na Chama Kikuu cha
Ushirika Mkoani Kilimanjaro(KNCU) kupitia mwenyekiti wake Ndugu Menald Swai
kilitoa msaada wa shilingi milioni moja, kampuni ya MONOBAN ya jijini Arusha
iliyotoa tani nne za unga na shilingi milioni moja za kununulia maharage zilizokabidhiwa na Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Ndugu Godfrey Mollel.
Misaada hiyo tayari imeshasambazwa katika kata za Machame Weruweru,Machame Kusini,Masama
Rundugai,Masama Mashariki,Masama Magharibi na Masama Kati.
Wafanyakazi wa kampuni ya vinywaji baridi Bonite Bottlers wakishusha moja ya magunia ya chakula kilichotolewa kama msaada kusaidia waliopatwa na maafa
Mkuu wa wilaya ya Hai ndugu Novatus Makunga akipokea msaada wa mabati kutoka kwa mwakilishi wa bonite kwa ajili ya kusaidia watu waliokumbwa na maafa ya upepo
No comments:
Post a Comment