Monday, February 17, 2014

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AANZA KUTATUA MGOGORO WA KADCO NA WANANCHI

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ASULUHISHA MGOGORO WA KADCO NA WANANCHIMkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Leonidas Gama



MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ASULUHISHA MGOGORO WA KADCO NA WANANCHI
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ndugu Leonidas Gama akizungumza na wananchi wakati wa kusuluhisha mgogoro kati ya wananchi na kampuni ya KADCO



MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ASULUHISHA MGOGORO WA KADCO NA WANANCHI

 Kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro ndugu Leonidas Gama na Mbunge wa Jimbo la Hai Mh. Freeman Mbowe wakiwasikiliza wananchi

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ASULUHISHA MGOGORO WA KADCO NA WANANCHI

Mkuu wa wilaya ya Hai Ndugu Novatus Makunga akizungumza na wananchi wa kata ya KIA, na Masama Rundugai wakati wa kusuluhisha mgogoro kati ya wananchi hao na kampuni ya KADCO
MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ASULUHISHA MGOGORO WA KADCO NA WANANCHI

Mbunge wa Jimbo la Hai Mh. Freeman Mbowe

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ASULUHISHA MGOGORO WA KADCO NA WANANCHI

Mbunge wa Jimbo la Hai Mh. Freeman Mbowe akieleza namna anavyojua historia ya mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ASULUHISHA MGOGORO WA KADCO NA WANANCHI
Mbunge wa Jimbo la Hai Mh.Freeman Mbowe akisalimiana na Wananchi baada ya mkutano huo kumalizika

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ASULUHISHA MGOGORO WA KADCO NA WANANCHI
Mwananchi wa kata ya KIA akitoa maelezo juu ya historia ya mgogoro kati yao na KADCO


Mkuu wa Mkowa wa Kilimanjaro ndugu Leonidas Gama ameuagiza uongozi wa KADCO kutowazuia wananchi waliokuwa wanalima na kulisha mifugo katika eneo lenye mgogoro hadi pale ambapo maamuzi juu ya mgogoro wao utakapotolewa.


Agizo hilo alilitoa baada ya kukutanisha pande hizo mbili na kusikiliza maelezo yao kwa nyakati tofauti juu ya mgogoro wa ardhi kati ya Kampuni hiyo na wakulima na wafugaji .

kwa upande mwingine amewataka wananchi kutofanya ujenzi wa nyumba za kudumu  katika eneo hilo mpaka watakapopata taarifa kamili ya maamuzi yatakayotolewa baada ya kupitia nyaraka mbali mbali zinazoonyesha kuwa KADCO ni wamiliki halali  wa eneo hilo na kupitia taarifa za wananchi walizotoa kwa kuzingatia  historia na uasilia wa eneo hilo.

Naye Mbuge wa Jimbo la Hai Mh Freeman Mbowe amewataka wananchi hao kuwa wavumilivu wakati tatizo lao linashughulikiwa na kuwaahidi kulifikisha suala hilo Bungeni endapo halitapata suluhu ya kudumu.

Hata hivyo amesema hapingani na uwekezaji kwakuwa ni suala lisiloepukika katika kuleta maendeleo ila amewataka wanaokuja kuwekeza kufuata taratibu,  sheria  na kuwashirikisha wananchi katika hatua za awali ili kuzuia mgogoro unaoweza kujitokeza.

1 comment: