Wednesday, January 14, 2015

WENYEVITI WA VIJIJI, VITONGOJI NA WAJUMBE WA HALMASHAURI ZA VIJIJI WAAPISHWA


HAI

Na Edwin Lamtey

Viongozi wa serikali za mitaa ngazi ya vijiji na vitongoji wametakiwa kusimamia na kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneo yao, kutenda haki na kuikataa rushwa huku wakikumbuka ahadi za viapo vyao walivyo kula.

Hayo yamesemwa na Msaidizi wa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Grace Mwakiwiluli wakati wa kuapishwa kwa wenyeviti wa  vijiji, kata, pamoja na wajumbe wa serikali zao. Bi Grace amesema kuwa kiongozi bora ni yule anaye weka mbele maslai ya wananchi wake nakutenda kazi kwa haki na uadilifu huku akiilinda, akiitetea nakuiheshimu katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo inawapa mamlaka katika utendaji wao wakazi.

Awali akifungua kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Hai ndugu. Melkizedeck Humbe amewaagiza viongozi waliochaguliwa kusimamia ujenzi wa maabara, madarasa, uwepo wa madawati mashuleni pamoja na kupiga vita suala la utoro kwa wanafunzi.

 Aidha pia Humbe amesema kuwa kipindi cha kampeni kimekwisha na kuwa huu ni wakati wa kufanya kazi bila kujali itikadi za vyama wala dini ya mtu huku pia akisema hatosita kuwa chukulia hatua kali zakisheria wale wote wata kao kiuka maadili ya kazi.

Naye mwenyekiti wabaraza la madiwani Halmashauri ya wilayaya Hai ndugu. Clement Kwayu amewapongeza wale waliochaguliwa katika uchaguzi uliopita waserikali zamitaa nakuwataka wote kushirikiana na viongozi wengine wakiwemo madiwani na watendaji wa kata na vijiji ili kuliletea taifa maendeleo zaidi.

Kwa upande mwningine baadhi ya wenyeviti  waliohapishwa wamewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi wote waliochaguliwa ili kuleta maendeleo katika maeneo yao hasa katika sekta ya elimu na miundo mbinu ya barabara.

Kuapishwa kwa wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji kunatokana na uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14 mwaka jana 

No comments:

Post a Comment