Monday, September 1, 2014

MH MWANGA ACHAGULIWA KUWA MAKAMU MWENYEKITI


Mh Twalibu A Mwanga Diwani wa Kata ta Masama Mashariki kupitia chama Cha Mapinduzi(CCM)  amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai .

Akiongea baaada ya kuchaguliwa Mh Mwanga amewataka madiwani wenzake kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano bila kujali itikadi zao za kisiasa kama walivyokuwa wakifanya hapo awali.

Alisema Baraza la Halmashauri la Hai ni la kuigwa na Halmashauri zote kwa kufanya kazi kwa ushirikiano  bila ya kujali itikadi za chama,licha ya kwamba baraza hilo lina wajumbe sawa kutoka vyama vya siasa vya CCM na CHADEMA.

"Halmashauri zingine zije zijifunze Hai,katika masuala ya maendeleo sisi hatuna chama tunafanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya watu wetu"alisema Mwanga.

Kabla ya uchaguzi huo kufanyika,aliyekuwa anashindania nafasi hiyo kupitia chama cha CHADEMA Mh Deogratius C Kimaro wa kata ya Masama Kati aliamua kujitoa kwa lengo la kumuachia mgombea wa CCM ili kuongeza ufanisis na ushirikiano zaidi kwa kuwa, tayari Mwenyekiti wa Halmashauri anatoka chama cha CHADEMA.

Akiondoa jina lake katika orodha ya wanaogombea katika uchaguzi huo Kimaro alisema"nimeamua kutoa jina langu ili kumwachia mwenzangu ateuliwe kuwa Makamu mwenyekiti,ili tuendelee kufanya kazi kwa ushirikiano kama ilivyo siku zote na kutoa nafasi kwa vyama vyote kuwa na ushiriki katika nafasi za uongozi"

Hii ni mara ya pili Mh Kimaro akijiondoa kwa dakika ya mwisho ya uchaguzi kwa lengo la kuachia nafasi hiyo ili pawepo na usawa wa uongozi kati ya CHADEMA na CCM katika Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Hai lenye wajumbe 22, kati yao 11 wakiwa ni CHADEMA na 11 wakiwa ni CCM.

No comments:

Post a Comment