Mwenyekiti
wa halmashauri ya Wilaya ya Hai Mh Clement Kwayu amewataka wananchi kutunza
miradi iliyopo katika maeneo yao kwa faida yao na vizazi vijavyo.
Mh Kwayu
aliyasema hayo katika kata ya KIA wakati
wa uzinduzi wa mradi wa maji unaoanza kutekelezwa katika vijiji vya kata
hiyo ikiwa pia ni mpango wa matokeo
makubwa sasa ambapo pia mradi huo unategemea kugharimu zaidi ya shilingi
bilioni tatu huku ukitarajiwa kukamilika mwezi
july mwaka huu.
‘Wananchi
wanapaswa kutambu kuwa maji ni uhai kwa
kiumbe yeyote yule na kila mwananchi anao wajibu wa kulinda miundo mbinu hiyo
maji ili huduma hiyo kupatikana kwa ukaribu na kwa wakati muafaka’alisema Mh
Kwayu
Kwa upande
mwingine Diwani wa kata ya KIA mh. Sinyoki pamoja na Mhandisi wa maji wa wilaya
Nyakaraita Mwita waliahidi kushirikiana bega kwa bega kuhakikisha kuwa
tatizo la maji katika ukanda wa tambarare linakwisha
Kwa upande
mwingine Meneja wa Bodi ya maji Uroki Bomang’ombe Mhandisi Prosper Shoo aliwashauri
wananchi wa Kijiji cha Kyeri kuifadhi mazingira kwa kupanda miti rafiki katika
vyanzo vya maji wakati wa ziara ya
uhamasishaji wa upandaji miti katika chanzo cha maji cha saaki katika maadhimisho
ya wiki ya maji.
Shoo alisema
kuwa kuna uharibifu mkubwa wa mazingira ambao unafanywa na wananchi hali
iliyopelekea maji kupungua katika chanzo hicho cha saaki huku akiiomba jamii
inayozunguka chanzo hicho kupanda miti ili kunusuru hali hiyo ambapo alisema
awali chanzo hicho kilikuwa kinazalisha maji ujazo wa 42m³ kwa
sekunde tofauti na sasa ambapo chanzo hicho uzalisha ujazo wa 41m³ kwa sekunde.
No comments:
Post a Comment