Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Hai imeidhinisha huduma ya Bima ya afya ya jamii kupitia mfukuko wa afya ya Jamii iliyoboroshwa (ICHF).
Mpango huo utatekelezwa kwa kushirikiana na shirika la
Farm acces kupitia mfuko wabima ya afya CHF kwa kushirikia na Halmashauri ya Wilaya
ya Hai ambao umelenga kumpatia mwananchi huduma ya afya kwa wakati wote na kumwepushia
gharama kubwa za matibabu.
Mpango huo
uliowakutanisha Madiwani na viongozi
wengine toka ndani ya Halmashauri umelenga kuboresha hali ya gharama ya afya kwa
Wananchi wa Wilaya ya Hai ili waweze pata huduma ya afya kwa kuzingatia kipato chake halisi.
Kwa upande wake Meneja wa Farm acces Majani Wambari alisema kuwa jambo la kuzingatia
katika utoaji huo wa huduma ya afya ni vema kwa watoa huduma hasa wauguzi kuwa
na hekima kwa kuwajali wanao tumia huduma ya afya pamoja na kuhamasisha watu
wengine kujiunga na mfuko huo kwaajili ya kukomboa afya ya familia.
Amebainisha
idadi ya wanao hitajika kupata huduma hiyo ya afya kupitia mfuko wa ICHF ni watu sita toka ndani ya kaya moja ambao
wataweza kunufaika na huduma hiyo ambayo ni baba,mama na watoto ambao wapo chini ya miaka kumi na nane na kwa wale ambao wana zaidi ya miaka kumi na nane lazima wawe wanafunzi.
Wambari Amekiri
kuwa wanapata changamoto kubwa wakati wa utoaji wa huduma ikiwa ni pamoja na
malalamiko ya wagonjwa wanao tumia bima ya afya kuto kusaidiwa kwa wakati
badala yake wanaofika na fedha mkononi ndiyo wanao pewa kipaumbele jambo ambalo
amelipinga na kuwataka wagonjwa kuripoti malalamiko hayo ili wanao toa huduma kinyume
kuchukuliwa hatua.
Naye
mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Clemence Kwayu aliwataka wajumbe wa halimashauri
hiyo kutumia mpango huo kuhamasisha Wananchi kujiunga kutokana na mfuko huo
kuwezesha kupunguza gharama ya matibabu.
“Kwanza
ikumbukwe ya kuwa ugonjwa huja ghafla hivyo kwa kutambua jambo hilo ni vema mtu
akajiwekea msingi mzuri wa taadhari kwa kujiunga na mfuko huu wabima ya
Afya,hii ni neema kwa wakazi wa Hai.”alisema Kwayu.
Amesema kuwa
jambo la kuzingatia ni kwa watoaji wahuduma katika vituo vya afya kuwa wazalendo
wakuhudumia wagonjwa kwa huruma na upendo ikiwa ni pamoja na kutumiautaalamu wao
wote wa mafunzo waliyonayo kuepusha malalamiko toka kwa wagonjwa.
Naye Mganga
Mkuu wa Hosipitali ya Wilaya ya Hai Paul Chaote alisema kuwa mapango huo utaanza kutumika
katika vituo vya afya vitakavyo pendekezwa ikiwa ni pamoja na hosipitali ya
wilaya ili kuboresha matibabu kwa wagonjwa.
Aliongeza
kuwa huduma hiyo inatarajiwa kuanza kutumika mwezi Mei mwaka huu ambapo
uhamasishaji na uandikishaji utaanza
rasmi kuanzia hivi sasa
“Natoa wito
na onyo kwa watoaji wa huduma nikimaanisha wauguzi wahosipitali ya Wilaya ya
Hai navituo vitakavyo tumika kutoa huduma hii ya afya kwa njia ya bima ya ICHF
kuacha mara moja kukiuka miiko na
maadili yakazi zao badala yake watoe
huduma pasipo ubaguzi wala lugha chafu kwa Wagonjwa ikiwa ni pamoja na
kuthamini muda mara baada ya mgonjwa kufika au kupokelewa jambo ambalo
litasaidia kuondoa lawama na kashfa juu ya watoa huduma.”AlisemaChaote
huduma hii utolewa kwa mwananchi kuchangia kiasi cha shilingi 25,000/ kwa mwaka na kumwezesha kupata huduma kwa mwaka mzima kwa familia yenye watu sita.
kwa upande wa serikali nao umechangia kiasi cha shilingi 25000,hivyo kufanya gharama halisi ya huduma hiyo kuwa silingi 50,000/= kwa kila kaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Hai Melkizedek Humbe wa kwanza kushoto,M/Kiti wa Halimashauri Clemence Kwayu wa pili kushoto,Makamu Mwenyekiti Ally Mwanga wakimsikiliza Meneja wa FarmAcces Majani Wambari juu ya mpango wamradi huo wa bima ya Afya
No comments:
Post a Comment