Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Hai akiwa ofisini kwake.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Hai akitoa zawadi kwa mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo
Afisa Tawala wa Wilaya ya Hai Bi Julieth Mushi akikabidhi zawadi kwa mmoja wagonjwa aliyelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Hai.
wauguzuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Hai wakiwa wamewasha mshumaa katika kuadhimisha siku ya wauguzi duniani
Mwenyekiti wa Chama cha wauguzi Wilayani Hai bi Rehema Antoni Pepin akiwa anatafakari kabla ya kuojiwa na waandishi wa habari
miongoni mwa wagonjwa walilazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Hai akipokea zawadi wakati wa maadhimsho hayo
wauguzi wa wakiwa wanatembelea wagonjwa katika kuadhimisha siku ya wauguzi duniani
Wauguzi hao walifikia maazimio hayo katika kuadhimisha siku
ya wauguzi Wilayani Hai iliyofanyika jana katika hospitali ya Wilaya ya Hai, ambapo
maazimio mengine ni pamoja na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na
watoto wenye umri chini ya miaka mitano, kuendelea kufanya kazi kwa ubunifu ili
kuboresha huduma kwa jamii nzima.
Akisoma risala ya wauguzi hao kwa mgeni rasmi bi Felicia Ritte alisema pamoja na changamoto
mbali mbali wanazokabiliana nazo wamefanikiwa kuongeza kwa idadi ya wauguzi
wasajiliwa toka 40 hadi 131 mwaka 2014, kupatikana
kwa jengo la upasuaji wa dharura hasa kwa akina mama, wauguzi wengi kupata
mafunzo rejea akitolea mfano PMTCT,PITC, ‘Quality improvement in health
Services, Human resource for health for management skilis, professional ethics
in health, family palinning, option B+ na infant feeding,’ na baadhi ya wauguzi
kupata nafasi ya kujiendeleza kielimu.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Hai ndugu Nyakaraita Mwita amewataka wauguzi kufanya kazi kwa weledi na
kufuata sheria, taratibu na kanuni za kazi akisisitiza wauguzi kuwa na huruma kwani kazi
hiyo imethaminiwa na jamii na serikali pia.
‘uguuzi umethaminiwa
, mnahitaji kukidhi kigezo cha kuwa na huruma kwakuwa kazi yenu inahitaji
huruma ,muache matumizi ya lugha chafu kwa wagonjwa na muwajali wagonjwa na kuwapenda’alisema
nyakaraita.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Hai ndugu Paul Chaote amesema
serikali imekuwa ikishughulikiwa tatizo la uhaba wa wauguzi ambapo kila mwaka
imekuwa ikiajiri wauguzi na kwamba mpaka sasa bado Hospitali ya wilaya imekuwa
ikikabiliwa na uhaba wa wauguzi kwa
asilimia 37.
Amesema licha ya upungufu huo wamekuwa wakifanya kazi kwa
kujituma na kwamba juhuudi hizo na ushirikiano wa watumishi wote wa Hospitali
hiyo imeifanya Hospitali hiyo kushika nafasi ya nne kitaifa katika hudma ya
utoaji chanjo.
wilwyw yw Hai Mko juu
ReplyDelete