WANANCHI wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro wametahadharishwa kuwa makini na kujikinga na mbu anayeeneza ugonjwa wa dengue kutokana na Wilaya hiyo kuwa na viashiria vya ugonjwa huo .
Tahadhari hiyo imetolewa na Madaktari kutoka Hospitali ya Wilaya ya Hai kufuatia kuwepo na taarifa ya watu wawili wenye viashiria vya ugonjwa huo ambao umekuwa tishio kwa wananchi wengi tangu uliposhika kasi ukianzia jijini Dar Es Salaam.
Wakizungumza katika Kituo cha Redio Boma Hai FM madaktari wa Hospitali ya Wilaya hiyo Dkt Julias Massawe na Happynes Ndenshau walisema mpaka sasa kuna viashiria vya ugonjwa huo kuwepo Wilaya hapa kutokana na watu wawili kusadikiwa kuwa na viashiria vya ugonjwa huo
Dkt Massawe alisema watu hao wawili ambao mmoja anasadikiwa kuwa alitokea jijini Dar Es Salaamu ambaye ni mkazi wa kijiji cha Narumu na mwingnine ni alitokea Arusha ambaye ni mkazi wa mtaa wa Kibaoni na kwamba vipimo vyao vimepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Alisema kutokana na watu hao kuwa na viashiria vya ugonjwa wa Dengue na kulazwa katika Hospiali ya St Jose ya mjini Moshi kufuatia hali hiyo Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari mapema pindi wanapohisi kuwa na dalili za ugonjwa huo kwa kufika katika kituo cha afya kilichopo karibu ili waweze kupatiwa huduma.
Nae Dkt Ndenshau alisema hatua zilizochukuliwa hadi sasa ni kutoa elimu kwa wataalam wa afya waliopo katika vituo vyote vya afya ili wanapobaini mtu mwenye dalili ili wanapoona mtu mwenye dalili hizo hatua zichukuilwe mapema ikiwa ni pamoja kupeleka vipimo vyake katika Hospitali ya Wilaya kwa hatua zingine zaidi.
Hatua zingine zilizochukuliwa na Uongozi wa Hospitali hiyo ni pamoja nakutoa elimu kwakutumia njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na kituo cha Redio Boma Hai FM, matangazo ya barabarani kwa kuwasisitiza wananchi juu ya usafi wa mazingira hasa kukata majani ,kutoacha madimbwi ya maji lakini pia kupiga dawa kwenye maeneo yenye miti mingi na hasa kwa wale ambao wamelima karibu na nyumba zao.
Alisema kwa sasa hakuna tiba
wala chanjo ya ugonjwa huo, hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari dhidi
ya maambukuzi ya magonjwa yanayosababishwa na mbu.
“mbu wanaoeneza Dengue ni Aides na si anofelis kama
jinsi baadhi watu wanavyosema kwani mbu huyo hueneza malaria,mbu hawa ung’ata mchana hivyo ni vema
wananchi wakachukua tahadhari kwa kuvaa nguo ndefu,kwa wanao lala mchana walale
kwenye neti na kuteketeza mazalia ya mbu’alisema Dk. Ndenshau.
Alizitaja dalili za ugonjwa
huo kuwa ni kuumwa kichwa hasa sehemu ya mebele karibu na macho,kichefuchefu,kutokwa
na upele mdogomdogo mwilini ,kutokwa na damu sehemu za wazi za mwili.
Kuhusu Madaktari hao wamewataka wananchi kufika katika kituo chochote cha afya kwa ajili ya
vipimo mara tu watakapohisi dalili kama walizozitaja kwa ajili ya kupata huduma
na kuwatoa hofu wananchi wasio kuwa na uwezo wa kulipia gharama za matibabu
kuwa vipimo vya ugonjwa huo vinagharamiwa na serikali kwa watakao gundulika
wana dalili za ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment