Akizungumza katika Baraza la Halmashauri hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Hai ndugu Novatus Makunga amesema tayari ameshawagiza Maafisa Kilimo ambao wameonana na wakala wa eneo husika na
kuchukua sampuli ambazo zitafanyiwa
uchunguzi.
Amesema pia wamewasiliana na tawi la SICO Arusha ambao
wamesema tayari wameshafanyia uchunguzi na kusema kuwa mbegu hizo ni bora
lakini Serikali lazima ijiridhishe baada ya uchunguzi unaofanywa na wakala wa mbegu Tengeru mkoani
Arusha kukamilika.
Hata hivyo amesema
mbegu zinaweza kuacha kuota kutokana na kukaa kwa muda mrefu ardhini na kukosa
unyevu nyevu na baadaye kuoza au mbegu kokosa ubora suala ambalo litathibika
baada ya uchunguzi kufanyika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Mh Clement Kwayu amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa hatua zilizochukuliwa na kumtaka aendelee kufuatalia suala hili kwa ukaribu zaidi.
Katika hatua nyingine Baraza hilo liliwaagiza wataalam wa Kilimo wa ngazi zote kuhakikisha kuwa wananchi wanapatiwa elimu ya kutosha juu uzuiaji wa viwavi jeshi ambavyo vinaripotiwa kuwa katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya Hai na Mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.
Akielezea hatua ambazo tayari zimechukuliwa Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika ndugu Lalashoi Kweka alisema tayari Idara imeshawasilisha taarifa katika ngazi mbali mbali ikiwa ni Mkoani na Wizarani na kuwasiliana na taasisi mbali mbali zinzofanya utafiti wa wadudu waharibifu wa mazao ambapo serikali imetoa kiasi cha lita 80 za dawa aina ya Elthrin 25 EC lita 80 kwa ajili ya kasaidia familia zisizo na uwezo wa kununua dawa za kuangamiza viwavi jeshi.
Hata hivyo amesema juhudi bado zinafanyika za kuhamasisha na kuelimisha wananchii juu ya aina ya dawa zinazotakiwa kutumika kili kuangamaiza wadudu hao waharibifu na kwamba elimu hiyo imetolewa na wataalam kupitia kituo cha Redio Boma Hai FM kinacho milikiwa na Halmashauri na kwamba hali si mbaya sana kwani wananchi wengi wameshapiga dawa.
No comments:
Post a Comment