Mmoja wa wajumbe wa ALAT Mkoa wa Kilimanjaro akisaini Kitabu cha wageni katika chumba cha mahabara katika shule ya Sekondari Udoro

Wajumbe wa ALAT Mkoa wa Kilimanjaro wakisikiliza maelezo juu ya ujenzi wa Jengo hilo la mahabara lenye miundombinu ya kisasa
Hivi ni baadhi ya vifaa pamoja na madawa yanayotumika katika mahabara ya shule ya sekondari Udoro
Wajumbe wa ALAT Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa nje ya Jengo la Mahabara la Udoro Sekondari
Baadhi ya wajumbe wa ALAT wakiangalia skimu ya umwagiliaji Kikavu chini
Katikati ni mtaalam wa Kilimo Noah Kajigili akimfafanulia mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai juu utekelezaji wa skimu ya umwagiliaji Kikavu chini
Wakulima wa Kijiji cha Kikavu chini wakimwelekezza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha wakati wa ziara hiyo ya ALAT
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai akiangalia sehemu ya skimu hiyo ya Kikavu chini
Wajumbe wa ALAT Mkoa wa Kilimanjaro pamoja nabaadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kikivu chini wakielezewa jambo la Mtaalam wa kilimo ndugu Kajigili
Wananchi wa Kikavu chini kupitia Ushirika wa wamwagiliaji (UWAKICHI) wameishukuru Serikali kwa ukarabati miundombinu ya skimu ya maji wa umwagiliaji wa Kikavu chini ambao umekuwa mkombozi wa wakulima katika Kijiji hicho.
Akisoma Taarifa ya ushirikia huo mbele ya Kamati ya ALAT Mkoa wa Kilimanjaro,ndugu Hemed Mghamba alisema kwa mwaka 2008/2009 skimu hiyo ilipata kiasi cha shilingi 30,701,390 kutoka ruzuku ya uwekezaji(DADG) kupitia DADP's kwa ajili ya ukarabati wa mita 620 za mfereji huku jamii ikiwa imechangia kiasi cha shilingi 6,947,292 na chama cha UWAKICHI kikichangia kiasi cha shilingi 500,00 na kwa mwaka wa fedha wa 2009/2010 skimu hiyo ilipokea kiasi cha shilingi 300,000,000 kutoka mfuko wa kuendeleza Umwagiliaji Wilayani(DIPF) huku jamii ikiwa imechangia kiasi cha shilingi 44,580,000 kama nguvu kazi huku mwaka 2011/2012 skimu hiyo ilipokea kiasi cha shilingi 100,000,000 kutoka katika Mfuko wa kuendeleza Umwagiliaji wilayani (DIDF)na jamii ikiwa imechangia kiasi cha shilingi 5,000,000 kama nguvu kazi fedha ambazo zimesaidia kukarabati skimu hiyo.
Alisema kutokana na ukarabati wa skimu hiyo wameongeza eneo la Umwagiliaji kutoka Hekta 421 mwaka 2008 hadi Hekta 541 ambapo wakulima wamewawezesha kuongeza uzalishaji wa chakula kwa kwamba kwa sasa wanavuna tani 3.75 za mahindi kutoka tani 2.5 za awali,mpunga tani 5.5 kutoka tani 2.9 za awali,na maharage tani 6 kutoka tani 3 za awali.
Alisema mbali na ukarabati wa skimu hiyo,kamati ya mradi imepata mafunzo kuhusu usimamizi wa mradi,taratibu za kuendesha Ushirika,usimamizi wa rasilimali ya maji,uendeshaji wa skimu na matengenezo,kilimo cha mahindi na maharage na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kamati ya mazingira ya kijiji na jamii kwa ujumla.
pamoja na shukrani hizo wamesema bato wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na ubovu wa miundo mbinu kwa maeneo ambayo bado hayajafanyiwa ukarabati na mmomonyoko wa maji ambapo ushirika huo unaendelea na jitihada za kuweka makinga maji na kupanda miti katika maeneo yenye mmomonyoko wa udongo.
ALAT Mkoa wa Kilimanjaro wapo Wilayani Hai kukagua miradi ya maendeleo ambapo tayari wametembeleo shule ya Sekondari Udoro kukagua ujenzi wa Jengo la Mahabara na ukarabati wa nyumba ya mtumishi na baadae walielekea katika Kijiji cha Kikavu chini kukagua skimu ya umwagiliaji ya Kikavu chini.
No comments:
Post a Comment