Friday, April 25, 2014

BARAZA LAFUKUZA KAZI WATUMISHI WATANO



Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya hai,hivi karibuni  limefikia uamuzi wa kufukuzisha kazi  watumishi wake watano kwa kosa la utoro kazini.

Maazimio ya kufukuzwa kazi kwa watendaji hao yamefikiwa baada ya Baraza hilo kujadili kwa muda mrefu na kujiridhisha  juu ya taarifa iliyowasilishwa kwao juu kutoripoti kazini kwa watumishi hao ambao baadhi yao wamekwenda masomoni bila kufuata taratibu.

Madiwani hao wamesema watumishi hao ambao wamefukuzwa watakuwa fundisho kwa baadhi ya watumishi wenye tabia kama hizo na wasiofuata taratibu,kanuni na sheria za utumishi wa uma na kutaka hatua hizo kuchukuliwa kwa watumishi wengine wenye tabia kama hizo na hasa katika ngazi za kata na vijiji.

Akizungumza kwenye Baraza hilo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Melkizedeki Humbe alisema watumishi hao wamefukuzwa kazi kwa kuzingatia  sheria namba 57(1) kifungu kidogo cha kwanza kwamba mtumishi anapotoroka kazini kwa zaidi ya siku tano mfululizo bila taarifa anatakiwa kufukuzwa kazi.

Amesema kamati iliundwa  kwa ajili ya uchunguzi na kuwapa nafasi ya kujitetea kwenye kamati ambapo kuna waliojitokeza na wengine hawakujitokeza na waliojitokeza pia utetezi wao haukukubalika ndipo umauzi huo  wa kuwafukuza ulipofikiwa

No comments:

Post a Comment