Wednesday, February 26, 2014

MKANDARASI M/S DENICO AKABIDHIWA RASMI MRADI WA MAJI KWA AJILI YA UTEKELEZAJI



Hili ni tenki la Mungo wa mae la  kupunguza nguvu ya maji, (PRT)eneo hili ndipomkandarasi M/s DENICO anatarajia kuanzia kazi



Kaimu Mhandisi wa maji ndugu E Kessy akimwelekeza mkandarasi kutoka  M/s DENICO   eneo analotakiwa kuisha katika lot1



 Eneo hili ndipo lilipojengwa tank la kupunguza kasi ya maji(PRT) la Somali ambapo mkandarasi wa LOT 1 anatarajiwa kuishia.





 watumishi wa Idara ya Maji pamoja na Mh Diwani wa Kata ya KIA wakimwelekeza Mkandarasi wa Kwanza kutoka kushoto ramani atakayotumia katika kutekeleza mradi wa maji

Wataalam, Mkandarasi pamoja na waheshimiwa Madiwani wa Kata ya KIA na Kata ya Machame Magharibi   wakiangalia tenki la maji Sanya Station.


 Wakwanza kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya KIA  mh OleNairuko Sinyoki na wapili kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Machame Magharibi Mh B .Kileo akifungua kilula cha maji katika kijiji cha Tindigani.



Mchumi Leonard Luwavi akiangalia moja ya kilula cha maji katika kijiji cha Tindigani


Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro katika kutekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN ) umemkabithi mkandarasi kutoka kampuni ya M/S Denico ya jijini Arusha kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji ya loti one unaoanzia katika kijiji cha Losaa hadi eneo la makazi ya wasomali  ili kuanza kuutekeleza mradi huo.

Akikabidhi mradi huo kwa mkandarasi, kaimu mhandisi wa maji wa wilaya Eliyona Kessy alisema mradi huo unatarajiwa kugharimu zaidi y ash. 1.1 2 bilioni na unaanzia kwenye tank lamaji  la Mungo wa Mae hadi kufikia tanki la maji la Somali settlement.
Kessy alisema mkandarasi anatakiwa kukabidhi mradi huo kwa halmashauri ukiwa umekamilika kabla ya mwaka wa fedha 2013/2014 kumalizika juni 31 mwaka huu na kwamba mradi huo una zaidi ya km.16.
Alisema fedha zilizotumika katika utekelezaji huo ni fedha kutoka wizara ya maji kupitia program yake ya maji na usafi wa mazingira vijijini .
“chanzo cha fedha zilizotumika katika mradi huu ni fedha kutoka wizara ya maji ambayo wizara ya maji kwa sasa inatekeleza program ya maji na usafi wa mazingira vijijini na hivyo ikaona umuhimu wa maji katika vijiji hivi” Alisema Kessy.
Alisema lengo haswa la kuanzishwa kwa utekelezaji huo ni kuwaondolea adha ya upatikanaji wa huduma hiyo wakazi wa ukanda wa tambarare ambao  wamekuwa wakitumia maji ya mito na mifereji ambayo kwa kiasi kikubwa yameonekana kuwa na madhara makubwa kwa afya zao ikiwemo watoto kuzaliwa na ulemavu wa viungo mbali mbali.
“Tunatekeleza mradi huu kwa maana ya kupeleka huduma ya maji katika ukanda wa tambarare wa Wilaya ya Hai kwenye vijijji vinne kikiwemo cha Sanya station, Mtakuja, Tindigani, na Chemka ambavyo havina maji safi na salama kwa kipindi kirefu sasa” Alisema Kessy.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya KIA OleNairuko Sinyoki ameishukuru serikali kwa kupeleka mradi huo katika kata yake ambayo  ilikuwa ina kabiliwa na tatizo la maji kwa muda mrefu .
“Naishukuru sana serikali kwa kupeleka maji kwenye eneo langu kwani kwa kipindi kirefu sana wananchi wa eneo langu hawana maji safi na salama lakini sasa naona neema imekuja kutuokoa kwa kiasi kikubwa sana” alisema Sinyoki.
Alisema kitendo cha kupatiwa maji pia kitaondoa wasiwasi kwa akina mama wa maeneo hayo ambao walitishia kugoma kubeba mimba kwa kile walichodai kuwa wanahofia kuendelea kuzaa watoto wenye ulemavu wa viungo mbalimbali kutokana na maji yaliyopo katika maeneo hayo.
“Yaani hivi sasa naamini hata migogoro ya ndani ya familia itapungua kwani  akina mama wataendelea kuzaa kutokana na tatizo hilo la maji ambalo lilionekana kuathiri sana kutokana na maji hayo kuwa na floride nyingi ambayo inasababisha watoto wengi kuzaliwa wenye ulemavu sasa limepatiwa ufumbuzi” Alisema diwani huyo.

No comments:

Post a Comment